ASSAs

STEVE NYERERE AKERWA NA KAULI ZA WADAU JUU YA MKUTANO WA RC PAUL MAKONDA

785
0
Share:

Msanii wa Filamu Bongo, Steve Nyerere ameonyesha kukerwa na kauli ya baadhi ya wadau (wasanii) kuwa hawakuitwa kwa utaratibu maalum kwenye mkutano ya juzi kati yao na Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkutano kati ya RC Makonda ulilenga kufahamu changamoto za wasanii na kutafuta namna ya kuzipatia ufumbuzi.

“Tukuite kwa utaratibu maalium wewe nani?, kwa hiyo Mkuu wa Mkoa aje akunyenyekee wewe?. Hivi Rais akikuita unamwambia mbona hukuniita kwa utaratibu maalum?,” amehoji Steve.

Moja ya mambo yaliyoafikiwa kwenye mkutano huo ni ujenzi wa ukumbi kwa ajili ya matamasha na maonyesho ya wasanii, inaelezwa kuwa ukumbi huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 20,000.

(Visited 55 times, 1 visits today)
Share this post