ASSAs

FC Barcelona wamemuongeza Lionel Messi El Clasico

376
0
Share:

Moja kati ya game itakayochukua headlines katika soka February 6 2019 ni pamoja na game ya FC Barcelona dhidi ya Real Madrid ambayo imezoeleka kwa jina la El Clasico, hii ndio game inayoongoza na kupendwa zaidi katika soka la Hispania kulingana na nguvu za club hiyo.

Awali FC Barcelona iliripotiwa kuwa na mashaka kuwa huenda staa wao Lionel Messi hasipate nafasi ya kucheza game hiyo ya Copa del Rey kwa sababu ya kuwa na majeraha, game hiyo ya nusu fainali itakayochezwa saa 23:00 kwa saa za Afrika Mashariki Lionel Messi atakuwepo pia.

Lionel Messi ambaye ni nahodha wa FC Barcelona aliumia nyama za paja Jumamosi iliyopita katika mchezo wa FC Barcelona dhidi ya Valencia, game ya LaLiga ambayo ilimalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, magoli yote ya Barcelona yakifungwa na Lionel Messi ila kuliwa kuwa na hofu ya staa huyo kukosa El Clasico

(Visited 23 times, 1 visits today)
Share this post