ASSAs

MIAKA 42 YA CCM NDG. LAILAH NGOZI (MCC) AWAASWA WANAWANA CCM WA MKOA WA DODOMA KUSHIKAMANA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU

1791
0
Share:

Mjumbe Wa Kamati Kuu Ya Halmashauri kuu Ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndg Lailah Ngozi jana Tarehe 5 Februari, 2019 ameanza ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Dodoma

Ikiwa ni siku ya kwanza wilayani Kondoa mjini na Vijijini Ndg Lailah Ngozi Amekagua uhai wa Chama na kuzungumza viongozi wa Chama kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya hadi Mkoa lengo ni kutoa semina ya namna bora ya kushiriki vyema na kukipatia Chama cha Mapinduzi ushindi wa kishindo ifikapo kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

 

Katika kuazimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Ndg lailah Ngozi pia ameshiriki katika shughuli ya kijamii ya ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Bereko wilayani Kondoa akishirikiana na viongozi mbalimbali na wana CCM waliokuwepo katika sherehe hizo nakupanda miti katika eneo la Kituo cha Afya cha Bereko.

Aidha Ndg. Lailah Ngozi amewapokea wana Chama wapya wanaotokana na vyama vya Upinzani akiwemo Mwenyekiti wa Kata pamoja na Katibu wake na wana Chama wakiwaida wote ni wanachama wa CUF .

Ndg. Ngozi amewataka wana Chama wa CCM wa Mkoa wa Dodoma na hasa Wilaya ya Kondoa kushikamana na kuwa wamoja katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo katika Chaguzi zake zote zijazo za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani.

“Kama ambavyo Serikali yetu ya awamu ya tano ilivyojipambanua kufanya kazi kwa vitendo na kujipambanua kikamilifu katika utekelezaji wa Ilani kwa uadilifu na umakini mkubwa, wajibu huo ni muendelezo wa kuitafsiri imani ya CCM kwa matendo na ndio maana hata kaulimbiu yetu ya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM inatoa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Hivyo ni wasihi tuendelee kuiunga mkono Serikali yetu ya CCM na pia kuendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM Dr. John Pombe Magufuli ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukachapa kazi kwa bidii na uadilifu .” Aliyasema hayo Ndg. Ngozi

 

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma aliwataka wana CCM na wananchi wote kupuuzia uzushi na uchochezi unaoenezwa dhidi ya wasioitakia mema Taifa letu. Napia alipata fursa yakuwaeleza umuhimu wa kuendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Uhuru pamoja na Muungano.

“Nchi yetu ni Nchi ya amani na ni miongoni mwa Nchi yenye utajiri mkubwa wa asili Duniani hivyo ni dhahiri maadui hawawezi kukosekana wapo na wataendelea kuwepo watatafuta kila mbinu kutudhoofisha kwa maslahi yao,kwa sasa wameminywa kila kona na Mzalendo Magufuli hivyo wameamua kutafuta kila njia kumtikisha lakini wamegundua kuwa Rais Magufuli ni mwamba imara usiotikisika..Tuendelee kumuombea kheri Rais wetu b kelele za mabwanyenye au mawakala wao.” Aliongeza Ndg. Ngozi

Ndg. Ngozi aliwashukuru wana CCM na wananchi wote wa Wilaya ya Kondoa kwa mapokezi makubwa na kujitoa kwao kujumuika katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

(Visited 163 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us