ASSAs

MBUNGE LUGIKO AWAFUNDA WASOMI VYUO VIKUU, AWATAKA KUBADILI MITAZAMO

1913
0
Share:

Mbunge  wa Bunge la Afrika Mashariki Happiness Elias Lugiko na Mjumbe Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji Bunge la Afrika Mashariki akizungumza Wakati kongamano Iiliyoandaliwa na wabunge watanzania wa Bunge la Afrika Mashariki katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam Tarehe 6 Februari.

Aliongelea suala la vijana kufikiria kujiajiri pia, kuliko kutegemea kuajiriwa tu.
“Wawe na mtazamo wa kuja kuajiri wengine kuliko kuwa na mtazamo wa kuja kuajiriwa tu. Hii ni kwa sababu ya upungufu wa ajira, kwa maana idadi ya watu wanaohitimu Chuo kwa mwaka ni wengi kuliko idadi ya ajira zinazotengenezwa kwa mwaka.”
Alisema ni aibu kwa Kijana kumaliza shule alafu unakaa mtaani tu hafanyi chochote alafu unaanza kuomba hela kwa mzazi nahali yeye alikusomesha akitegemea ukihitimu umsaidie, maana aliuza hadi ng’ombe na mashamba ili akulipie Karo.

Pia aliongeza “Vijana wasiwe watu wa kuilalamikia selikali tu eti haiwapi ajira na hali uhalisia ndo huo ajira chache. Na mtazamo wa kuona watu wanaofanya biashara ni watu wasio na elimu au waliokosa ajira sio mtazamo mzuri. Kwani wapo watu wasomi, na waliamua kufanya biashara badala ya kuajiriwa, sio kwa sababu walikosa ajira, la hasha, Ila waliamua wawe waajiri na sio waajiriwa.”
Mh Mbunge alitolea Mfano wa Watu kama akina Reginald Mengi, Mohamed Dewji na wengine wengi tu hapa Tanzania.
Hata kwa wale Hawana elimu kubwa, wanaweza kufanya biashara na wakaajiri wengine. Tunayo mifano ya watu ambao Hawana elimu kubwa ila wameajiri wasomi wenye elimu kubwa.

Mheshimiwa alisema yeye alipomaliza Chuo tu akaanza kujishughurisha na biashara, na hata alipoingia kwenye ajira, hakuacha biashara, bali aliendelea kuifanya kwa muda wa ziada baada ya masaa ya kazi za mwajiri wake hadi Leo anaendelea na biashara pia.
Tukifanya hivi sasa, miaka ijayo nchi yetu haitakuwa na uhaba wa ajira.

Pia aliongelea kuhusu fursa zinazopatikana katika jumuia ya Afrika Mashariki na kwamba Tanzania ina Nafasi kubwa ya kunufaika nazo.
Alisema mazao ya chakula kama mchele, mahindi, matunda na mbogamboga za majani zina soko kubwa katika nchi wanachama wa wa Afrika Mashariki.
Mfano wakenya huja kununua mahindi Tanzania, wanaya-process alafu wanauza unga nchi za nje, na wakiwa kule hawawezi kama mahindi yanatoka Tanzania. Na tukiangalia hata katika mipaka ya Tanzania iko na hali hii, ilitakiwa bize kibiashara ili kukamata masoko ya nchi jirani. Mpaka kama waRusumo ni vyema ujengwe uwe soko kubwa kama kariakoo, maana watu hutoka Congo kuja Dar as salaam kuchukua bidhaa, nahali kama pale mpakani pangekuwepo na soko kubwa tungeuza zaidi. Sasa kwa sababu ya umbali wengine huishia Rwanda kununua bidhaa ambazo warwanda huzitoa Tanzania.
Tanzania tuchangamkie fursa.

(Visited 217 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us