ASSAs

TAARIFA MPYA KUHUSU KUTAFUTA MWILI WA EMILIANO SALA

428
0
Share:

Kikosi kazi kinachoendesha zoezi la utafutaji wa miili ya mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala pamoja na rubani wake David Ibbston waliyepotea na ndege ndogo binafsi siku ya January 21 2019, wakiwa angani kurejea Cardiff Wales wakitokea Nantes nchini Ufaransa.

Baada ya zoezi hilo kuchukua muda mrefu na ndege iliyokuwa imewabeba kukutwa chini ya bahari, iliripotiwa kuwa mwili mmoja umekutwa chini ya bahari ila kutokana na kuharibika vibaya haujajulikana ni mwili wa nani kati ya Emiliano Sala na rubani wake David Ibbston.

Leo imeripotiwa kuwa mwili huo umefanikiwa kutolewa chini ya bahari na kukupakiwa katika Ambulace kwa ajili ya kuupeleka Mahabara kuufanyia uchunguzi zaidi ni mwili wa nani kati ya Emiliano Sala na rubani wake.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Emiliano Sala ambaye ni raia wa Argentina, alikuwa mchezaji wa Cardiff City aliyejiunga na timu hiyo mwezi huu January akitokea Nantes FC ya Ufaransa kwa ada ya pound milioni 15 lakini kwa bahati mbaya walipotea na ndege wakiwa njiani kurudi Cardiff akitokea Nantes ikiwa ni siku mbili zimepita toka asaini na timu hiyo.

(Visited 31 times, 1 visits today)
Share this post