ASSAs

BONNAH : KUNA BAADHI YA WATENDAJI SIYO WAAMINIFU

1128
0
Share:

Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh Bonnah Ladislausia, amesema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serekali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora lakini kuna baadhi ya watendaji siyo waaminifu katika utoaji wa huduma bora.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam, alipokua katika mkutano wa kikazi na wananchi wa kata ya Vingunguti wakati akijibu kero ya baadhi wa wananchi hao, ambao wameilalamikia Serikali hasa katika sekta ya Afya ambapo waliahidiwa kupatiwa huduma bure wazee na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano lakini kwao imekuwa ndoto za upatikanaji dawa bure.

“Katika ziara tulioifanya na aliyekuwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt,Hamis Kigwangwala pamoja na Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile tumegundua Serikali imepeleka dawa kwa asilimia 94 aina mbalimbali katika vituo vyote vya Afya nchini ambapo makundi ya watoto na wazee wanatakiwa kupata huduma bure”amesema Bonnah

 

Naye mmoja wa wazee waliokatiwa bima ya Afya ili watibiwe bure amesema bima hizo zimekuwa kivuli, kwani kila anapokwenda kituo cha Afya kutibiwa anapimwa lakini Ddwa hapewi huambiwa aende dirishani akalipie, hivyo anashangazwa na kauli ya Rais John Magufuli kusema wazee na Watoto watubiwe bure.

Kwa upande wake, Diwani wa kata Omary Kumbilamoto amesema wanakabiliwa na changamoto ya maabara katika shule ya Sekondari Vingunguti pamoja na upungufu wa walimu wa sayansi pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa,kutokana na ufaulu wa wanafunzi kuongezeka.

“Tunachangamoto ya madaktari katika zahanati yetu ya Vingunguti kwa sasa tunapokea wagonjwa 180, hawa ni wagonjwa wengi kwa siku katika zahanati, ufinyu wa vyumba vya madarasa pamoja na miundombinu chakavu ikiwemo barabara ya Machinjio Vingunguti na mifereji ya kutiririsha maji ” amesema Kumbilamoto.

 

Amesema kuwa, wanatarajia kujenga machinjio ya kisasa na ya kimataifa Vingunguti, ambapo amemtaka mkandarasi yoyote atakae pata tenda hiyo,lazima achukue vijana wa kata hiyo ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi.

“Serikali imetupendelea sana katika kata yetu kwani imeongeza pesa kutoka shillingi bill 8.5 hadi shilling bill 12 na mill 300 kwa ajili ya kujenga machinjio ya kisasa na ya Kitaifa ” amesema Kumbilamoto

Hata hivyo, amemuomba Mbunge huyo, kuwasaidia akina mama wajane waliopo katika kata hiyo ambao wamejiunga kikundi kwa ajili ya kupata fursa na kuwa wajasiriamali lengo ni kujikwamua na hali duni ya maisha kutokana na walio wengi hawana uwezo wa kuendesha maisha yao.

(Visited 158 times, 1 visits today)
Share this post