ASSAs

DKT BASHIRU ASEMA CCM HAITAVUMILIA WATANZANIA KUGEUZWA MANAMBA.

1686
0
Share:

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ali Kakurwa leo 9 Februari, 2019 amefanya ziara kikazi ya siku moja mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Katika ziara yake Dkt Bashiru alipata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi wa wilaya ya Kilosa na kuzungumza nao ambapo alieleza yafuatayo:-

“Nimekuja Hapa Kilosa Hapa nimeitwa na Wananchi ambao Hawaridhishwi na Namna Ambavyo Suala ya Ardhi linashughulikiwa na Vyombo Vyenye Mamlaka na Mahusiano ya Wakulima na Mamlaka”

“Nimeambiwa kwamba Mashamba ambayo Yamefutwa badala ya Kuwa NEEMA yamezusha Balaa. Ardhi ndio kielelezo cha Uhuru wetu na Uhai wetu, Usimamizi Mbovu wa Ardhi ni Usaliti kwa wapigania Uhuru wa Nchi Yetu”

“CCM Haitamvumilia Mtu ambaye atawageuza Manamba Watanzania wengine na Yule Anamiliki Ardhi na Haiendelezi”

“Hakuna Kiongozi wala Tajiri Nchi Hii Ambaye Halishwi na Maskini ila Shukrani ya Punda ni Mateke. Namuomba Rais Wetu aanze kutibu Ugonjwa wa Deko unasomesha watu wanazunguka Kutukana nchi Yao na Rais wao kisa Ugonjwa wa Deko”

“Yupo Msomi Mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua Ugonjwa wa Deko, anadeka Hajui Jembe kwa maisha yake, hajui Mpunga unalimwaje wala Samaki wanavuliwaje. Hajapanda Bodaboda Muda mrefu na watoto wake Hawasomi Shule Hizi anazunguka dunia Nzima Kutuchafua”

“Ni Marufuku Kuvunja Haki za wazalishaji wadogo Hasa Maskini, Ni Marufuku kubadilisha Ardhi kuwa Bidhaa”

“Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini Tumewaamini tumewapa Dhamana ila ukiwatembelea Ofisini wanadeka, mara Nyingine Hawapo, wanajipendelea wao.”

“Zaidi ya Mashamba 40 Hati Zimefutwa Lakini ni Machache Ambayo Yamewekewa Mpango Mzuri wa Kuyagawa kwa Wananchi”

“Ugonjwa wa Kushiba na Kula Bure anamuita Rais wetu Hajui Kiingereza Mtu Mwenye Shahada Tatu Tena za Kemia na anaitwa Daktari wa kusomea sio Mitishamba. Lissu anasema Hajui Kiingereza na Hatembelei Nje kanakwamba Kachaguliwa na watu wa Ulaya.”

“Dalili za Ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni Kusema Uongo, dharau, Deko, Uonevu, Kiburi, Majivuno. ugonjwa Huu unaambukizwa na Tumeulea na Manesi na Madaktari wa Ugonjwa Huu ni Watanzania Nyie wenyewe”

“Huu Ugonjwa Hatari, unaambukizwa ni Hatari Kuliko Ukimwi. Anasema Tumeweka Kifungu kwenye Katiba ya CCM cha Kuzuia watu kugombea Urais Sio Kweli ni Uongo.”

“Dalili za Ugonjwa Huu Uongo, Deko, ubinafsi wa Kuota Urais wa Tanzania, mwenye Kiburi kwa Watanzania anaenda Ulaya kuzungumza Lugha za wakoloni Huyo anayemuita Dikteta amefuta Mashamba kwa ajili ya Wanyonge”

“Nilipomskiliza Nikasema ni Muongo na kwa Sababu a naumwa Ugonjwa unaitwa Tundu Lissu bhas Yupo Kwenye Hali Mbaya”

“Ugonjwa wa Tundu Lissu ni Hatari ila Unaponyeka amuache Rais atumikie Wanyonge, watendaji wote wa serikali ambao Hawataki Kupona Ugonjwa wa Tundu Lissu watafute Serikali Nyingine ajira Ni Hiari waandike Barua waseme Chama Hiki Hakipendi Dhuruma,Mimi Nadhurumu, Hakipendi Uongo Mimi Muongo uachie Madaraka”

“Tusipoangalia Nchi Hii itageuka ya Manamba, Tusiangalia Ardhi watu Hawa Watakula Nini na watoto watalala wapi. Amechagua Marekani Nchi ambayo imejengwa na Watumwa na Majengo Anayozungumzia Yamejengwa kwa Jasho la Watu Weusi”

“Nawaambia Hata Kwenye Chama Ugonjwa Huu Upo, Wanachama Hawasikilizwi, Dhuluma Zinaendelea Sipati Taarifa kutoka kwenye Chama Hadi Wananchi Wenyewe. Uhalali wa CCM kutawala sio Kuvaa Nguo za Kijani na nyimbo za Hiyenahiyena ni Kulinda Haki za wafanyakazi na wakulima “

“Naelekeza Nchi Nzima Viongozi wa Chama, Mabalozi, viongozi wa Matawi, Wenyeviti wa Kata, wilaya, Mikoa na Sekretariati zao lazima Tuweke Mfumo dhabiti wa Mawasiliano wa kushughulika na Shida za watu”

“Mimi Ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa Chama Kinachoongoza serikali mbili ya Muungano na Zanzibar, Huniongi Mimi, hunitishi wala Kunibabaisha. Ninayo Jeuri ya Mwenyekiti Wetu Taifa Niguse Uone”

“Vijana wa Kitanzania Someni na Muwe na Nidhamu sio Usomi wa Kuhongwa kusema Uongo. Tunataka wasomi wanaojali Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi”

“Mchango wa WASOMI Nchi Hii Haujawa Mkubwa sana Kama ule wa Wapigania uhuru ambao wengi walikuwa Hawajasoma”

“Vyombo vya Dola Visutumike Vibaya Kwenye Migogoro ya Ardhi. Polisi Msitumike Vibaya Kuzima Sauti za Wananchi Wanyonge wanaodai Haki Zao Za Msingi”

“Dkt Magufuli Ameingia kila Eneo ambalo linampa Nafuu Mwananchi Mnyonge, kila atakayejaribu Kukwamisha Juhudi Hizi Tutamung’oa”

“Sisi Kwenye Ilani Tumehaidi Kutokomeza Rushwa na Ufisadi. Viongozi Kemeeni Rushwa Tena Kwenye Ardhi Maana Ni Hatari Sana. Bora umwibie Mtu Mme au Mke atapata Mwingine ila Sio Ardhi Maana Ardhi ikishaondoka Imeondoka.”

“Ni Marufuku Nchi Nzima Halmashauri za Wilaya Kutoza Pesa na Kugeuza Ardhi kama Magulio. Kuna Njia Nyingi za Kupata Mapato watu wakishiba watazalisha watalipa Kodi. Mapato Haya ya Kuchomekeana Hapana”

“Mmekosea Sana Halmashauri Kutoza Elfu 40 kwa Kila Mwananchi Kupata Ardhi Huo ni Unyarubanja Acheni Mara Moja. Hatuwezi kufuta Ada ya Elimu, halafu Upande wa Ardhi Tuweke gharama watoto wa Maskini wakose Chakula, tutakuwa Tunajichanganya.”

” Kazi Ni Kipimo cha Utu,Chapa Kazi Tulinde Uhuru na Utaifa Wetu”
Miaka 42 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi

(Visited 167 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us