ASSAs

SIMBA YAICHAPA 1-0 AL-AHLY NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUTINGA ROBO FAINALI

1228
0
Share:

Baada ya kucheza mechi ugenini bila kupata ushindi hatimaye leo Mnyama mkali kuliko wote msituni klabu ya Simba imewapa raha mashabiki wake kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kuifundisha soka Al-Ahly toka Misri na kuichapa bao 1-0 na kufufua matumaini ya kutinga hatua ya Robo Fainali Klabu bingwa Afrika.

Wakicheza mbele ya umati wa mashabiki na wapenzi wa soka nchi waliourika katika uwanja wa Taifa huku wakishangilia na kuimba WE CAN Simba walicheza kwa pasi za kuonana na kuwafanya Al-Ahly kucheza kwa kupoza mpira.

Hadi mapumziko timu zote zilikwenda mapumziko bila nyavu kutisikika huku zikifanya mabadiliko kwa wachezaji wao lengo ni kupata ushindi Simba waliingia kwa kasi na kulishambulia lango la wapinzani kama nyuki.

Dakika ya 65 Mshambuliaji mwenye mapafu ya Mbwa Meddie Kagere aliwanyanyua mashabiki waliofurika wakiongozwa na Mohamed Dewji ‘MO’ akifunga bao safi baada ya kazi nzuri ya beki Zana Coulibaly alipiga love pasi liyotua kwenye kichwa cha John Bocco na akaweza kumtengea mfungaji wa bao hilo.

Baada ya kuingia kwa bao hilo Simba waliendelea kuipeleka chapuchapu Al-Ahly na hadi dakika 90 mpira unamalizika wenyeji wameibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha pointi 6 na kuchupa hadi nafasi ya pili huku Al-Ahly wakibaki na nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 9 kwa ushindi huo Simba wamefufua matumaini ya kutinga robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika huku wakiwaombea As Vita wafungwe ama watoke Sare na JS Saoura

(Visited 81 times, 1 visits today)
Share this post