ASSAs

SOS YAANDA SEMINA KWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI MEMKWA

802
0
Share:

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumane Shauri amewataka walimu wa shule ya msingi (MEMKWA) wasiangalie maslahi yao binafsi badala yake wawekeze nguvu zao kwa wanafunzi wanaowasomesha ili waweze kuleta matokeo chanya na kuongeza ufaulu katika mitihani yao.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam, wakati walipokua akifungua semina ya siku 14 ya kuwajengea uwezo walimu wa shule ya msingi wanaofundisha watoto wenye mazingira magumu (MEMKWA) ambayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali (SOS).

Amesema kuwa, katika Manispaa ya Ilala watoto wengi walikua wapo mtaani wakizurura na kuombaomba barabarani lakini wameandaa utaratibu maalum wa kuhakikisha watoto wote wanapata elimu na wale waliokua wanatoka mikoa ya jirani wamewarudisha katika mikoa yao.

Ameongeza kuwa, lengo la Rais John Magufuli ni kuwaona watoto wote wanakwenda shule ndio maana akaweka elimu bure, hivyo mewataka walimu hao kufanya kazi vizuri na kuwahakikishia changamoto zao atazitatua ikiwemo kuwalipa madeni yao.

Kwa upande wake, mratibu wa mpango wa kucheza na kusoma kutoka shirika la SOS, Saraphina Lelo amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo na kuwaongezea ufanisi zaidi walimu wa (MEMKWA) katika kuwasomesha watoto hao.

“lengo la semina hii ni kuhakikisha walimu hawa wanapata mafunzo ya kutosha na kuelewa namna gani wanaweza kuwahendo watoto hawa na kuongeza ufaulu katika Manispaa ya Ilala katika kata Chanika na Zizingiwa”amesema Saraphina

(Visited 83 times, 1 visits today)
Share this post