ASSAs

MBUNGE MAVUNDE AWATOA MACHOZI YA FURAHA WAKINA WAJAWAZITO WA DODOMA MJINI

439
0
Share:

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo amewatembelea wakina mama wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia(Delivery Pack).

Mifuko ya Vifaa vya Kujifungulia yenye idadi ya 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa,hali iliyopelekea furaha kubwa kwa wakina mama wajawazito na kushindwa kuficha hisia zao na kudondosha machozi ya furaha.

    

“Nimeamua kuitumia siku ya leo kuonesha upendo kwa wakina mama wangu wa Dodoma kwa kusaidia vifaa hivi muhimu wakati wa kujifungua,hii ni shukrani nairudisha kwenu kwa upendo wenu mkuu kwangu”Alisema Mavunde.

Akimshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada huo mkubwa,Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dr Gatete Mahava amemuomba Mbunge Mavunde kuendelea kusaidiana na Serikali kutatua changamoto katika sekta ya Afya hasa katika kituo cha Afya cha Makole ambacho kimefanyiwa upanuzi mkubwa baada ya kukamilika ujenzi wa wodi ya wakina mama kupitia fedha kiasi cha Tsh 500m zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli katika Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya.

Katika tukio hilo Mavunde aliambatana na Viongozi wa CCM wilaya,Mbunge wa Viti Maalum Mh Bura,Madiwani wa Kata,Wasaniii na Mama Lishe wa Soko kuu Majengo.

(Visited 28 times, 1 visits today)
Share this post