ASSAs

RC MAKONDA AWATAHADHARISHA WASANII KUTOJIINGIZA KATIKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA.

383
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Wasanii kujiepusha na Matumizi ya Dawa za kulevya kwakuwa yatafifisha ndoto zao na kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

RC Makonda amesema wasanii wanapaswa kutambua kuwa hao ni kioo cha jamii hivyo wanaweza kuijenga jamii kama wakitumia vizuri nafasi yao na pia wanaweza kuharibu maadili Kama wasipotambua nafasi yao.

Mhe. Makonda ametoa rai hiyo jana wakati wa kongamano kuhusu tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii ambapo amesema anachoshukuru ni kuona kampeni aliyoanzisha imesaidia kuokoa vijana wengi waliokuwa wanaangamia kwa dawa za kulevya.

Aidha RC Makonda amesema kwa sasa hata upatikanaji wa dawa za kulevya umekuwa wa tabu kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na serikali katika kudhibiti biashara hiyo.

Katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya, wasanii na viongozi wa dini wamempongeza RC Makonda kwa moyo wa ujasiri wa kuanzisha Kampeni ya kupambana na dawa za kulevya iliyosaidia kuokoa vijana wengi.

Kongamano hilo la tatizo la dawa za kulevya limehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

(Visited 25 times, 1 visits today)
Share this post