ASSAs

TOTTENHAM HOTSPURS NA REAL MADRID WAPATA USHINDI LIGI YA MABINGWA ULAYA

406
0
Share:

Mshambuliaji Mkorea, Son Heung-min akishangilia baada ya kuifungia Tottenham Hotspur bao la kwanza dakika ya 47 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Wembley mjini London. Mabao mengine ya Spurs yamefungwa na Jan Vertonghen dakika ya 83 na Fernando Llorente dakika ya 86

Marco Asensio akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 87 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ajax kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Johan Cruijff Arena mjini Amsterdam. Real Madrid walitangulia kwa bao la Karim Benzema dakika ya 60 akimalizia kazi nzuri ya Vinicius Junior, kabla ya Ajax kusawazisha kupitia kwa Hakim Ziyech dakika ya 74 akimalizia pasi ya David Neres na kupata bao la pili lililofungwa na Nicolas Tagliafico akitumia makosa ya kipa Thibaut Courtois, lakini bao likakataliwa baada ya refa Damir Skomina kupata msaada wa marudio ya picha za video (VAR)

(Visited 22 times, 1 visits today)
Share this post