ASSAs

‘WASANII TUACHE UNAFKI WENGI WETU NI WANAFKI SANA’ SHILOLE

395
0
Share:

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Mjasiliamali wa kuuza Chakula Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ametoa neno kwa wasanii wenzake kwa kuwataka kuacha kukumbukana baada ya kifo.

Shilole amefunguka hayo siku ya jana katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Shilole amewajia juu baadhi ya wasanii ambao amediriki kuwaita wanafki na kudai wamejitokeza Baada ya kifo chake na kuanza kumposti na kudai wameguswa wakati kwenye uhai wake hakuna hata mmoja aliyeposti kazi zake.

“Mimi naona ni vizuri mtu akapewa heshima yake wakati yuko hai ili aone kama kuna watu wanampenda na kumjali sasa Leo hii amekufa ndio anapewa hio sapoti anajuaje sasa?” alihoji Shilole.

aliongeza kuwa, “Wakati yupo hai anatoa nyimbo hamposti wengine Mpaka wanatumia ngoma zake kama cover lakini bado hawamposti wala kumpa heshima yake kama legendari Ndio maana  mimi kila siku nasema wasanii tuache unafiki wengi watu ni wanafiki sana”.

Siku ya jana Msanii wa muziki wa hip hop nchini Godzillah alifariki dunia Baada ya kuugua ghafla nyumbani kwake Salasala. Wasanii mbali mbali walijitokeza kutoa pole na hata kumposti katika kurasa zao ya Mitandao ya kijamii.

(Visited 30 times, 1 visits today)
Share this post