ASSAs

WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI WAKATAA SIASA NCHINI HUMO

462
0
Share:

Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani, umetoa taarifa ya kwamba hawapo tayari kujishughulisha kwa namna yoyote ya shughuli za vyama vya  kisiasa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuaanda mikutano ya wanasiasa nchini humo.

Kupitia barua inayoaminika kuandikwa na kiongozi wa umoja huo, Ephraim Makanja imeeleza mbali na kuandaa mikutano, Watanzania waishio ujerumani hawaruhusiwi kufanya mapokezi ya viongozi wa kisiasa kwa kuwa wamepata taarifa kwamba wapo wanasiasa wanataka kuwageuza jukwaa la kisiasa.

Bw. Makanja ameeleza kwamba, anawaasa watanzania wanaoishi ujerumani kutotumika kwa namna moja ama nyingine katika kuandaa mikutano ya aina hiyo na kwamba umoja huo hautakubali kutumika kama jukwaa.

“Hatutaki mkutano na viongozi wa vyama vya kisiasa kwani sisi sio kambi ya siasa,” Imeeleza sehemu ya barua hiyo.

Tamko hili la Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani limekuja kiwa ni siku chache kupita tangu Mbunge wa Singida Mashariki , Tundu Lissu alipopata nafasi ya kuzungumza Washington DC na watanzania waishio nchini Marekani.

(Visited 41 times, 1 visits today)
Share this post