ASSAs

DC MURO AMSHANGAZA WAZIRI LUGOLA

1055
0
Share:

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kwa juhudi alizozifanya za kukarabati Gari ya Polisi aina Land Rover defender ambalo lilikuwa halitumika Kwa miaka Mongi Kutokana na kuchakaa na kuwa kama Chuma chakavu ambapo ukarabati huo umegharimu zaidi ya milioni 19

Mhe Lugora amesema Juhudi zilizofanywa na Dc Muro kuwezesha ukarabati wa Gari hiyo ambayo Imekarabitiwa na wadau wa maendeleo Wa wilaya ya Arumeru kutasaidia kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mamlaka ya mji mdogo wa Ngaramtoni.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amesema Kwa kipindi Cha miezi mitano alichotumikia wananchi wa Arumeru amemua kutatua changamoto za vifaa vya kutendea kazi Kwa jeshi la polisi ikiwemo kukarabati Magari yote ya Jeshi la polisi wilaya ya Arumeru Kwa kuwashirikisha wadau badala ya kusubiria fedha kutoka serikali kuu.

(Visited 100 times, 1 visits today)
Share this post