ASSAs

WAZIRI MKUU AWAONYA DC NA DED KUHUSU KUROGANA

2346
0
Share:

Kutokana na tofauti za kutoelewana  zilizopo kati ya  Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wawili hao Waende Ng’ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo leo Jumatano, Februari 20, 2019 wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya,

mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana.” amesema Waziri Mkuu

Aidha Waziri Mkuu amesema, “sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii.”

(Visited 1,111 times, 1 visits today)
Share this post