ASSAs

PAKA APEWA URITHI WA BILIONI 456

1903
0
Share:

Paka aliyekuwa akimilikiwa na  mkongwe wa mitindo Duniani marehemu Karl Lagerfeld ametangazwa kuwa mrithi wa mali zote za mkongwe huyo wa mitindo duniani.

 Choupette ndio jina maarufu la Paka huyo atamiliki utajiri wake ambao unatajwa kufikia zaidi ya shilingi Bilioni 456 za Kitanzania na inaripotiwa kuwa paka huyo alikuwa akilelewa kifahari na mmiliki wake tokea mwaka 2011.

Karl Lagerfeld aliyefariki Jumanne ya  Februari 19,2019 jijini Paris akiwa na umri wa miaka 85 akiwa miongoni mwa watu ambao walikuwa nyuma ya pazia ya mafanikio ya nembo kama Tommy Hilfiger, Chanel na Fendi mwaka 1980.

Umaarufu wa paka huyo umekuwa mkubwa hata katika mitandao ya kijamii, ambapo katika ukurasa wake wa Instagram unaoendeshwa na mtaalam wa masoko mitandaoni, Ashley Tschudin, umefikisha jumla ya wafuasi 120,000.

 

CREDIT; EATV

(Visited 260 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us