ASSAs

‘TULIKUTANA NA RUGE KWENYE MAZINGIRA YA KAZI’ ZAMARADI MKETEMA

2965
0
Share:

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba bado anaumwa na tukio linaloendelea kwa sasa ni Watanzani na marafiki wa bosi huyo kumuombea na kumchangia baada ya gharama ya matibabu kufikia tsh milioni 650.

Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wamekuwa waliwaalika wadau mbalimbali ambao wanaguswa na maisha ya Ruge na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu mwanaharakati huyo wa muziki wa Bongo Fleva.

Alhamisi hii amealikwa, Zamaradi ambaye ni mama watoto wa Ruge ambapo amefunguka mambo mbalimbali pamoja na namna alivyokutana na Ruge.

“Tulikutana na Ruge kwenye mazingira ya kazi, na mimi nimemjua Ruge kupitia Babu Tale. Tale ndio mtu ambaye alinitambulisha kwa Ruge kwa mara ya kwanza, alinipa namba yake akanimbia mtafute huyu bwana lakini usimwambie kama mimi ndiye niliyekupa namba,” alisema Zamaradi.

 

CREDIT;UDAKU SPECIAL

(Visited 434 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us