ASSAs

AJALI YA GARI YAUA 17 MKOANI SONGWE

2316
0
Share:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 19, baada ya kutokea kwa ajali ya gari  iliyohusisha gari aina ya Lori namba T 825 CMJ iliyoligonga gari lenye nambari T 269 CJC aina ya Coaster.

Akizungumza na chombo cha www.eatv.tv Kamanda Kyando ameeleza ajali hiyo imetokea usiku wakuamkia leo majira ya saa 3 usiku katika eneo lenye mwinuko mkali katikati ya mpaka Mbeya na Mkoa wa Songwe ambapo mpaka sasa jeshi hilo linaendelea kuhakikisha barabara ya sehemu ajali ilipotokea inaweza kupitika.

Ajali ilitokea mnamo majira ya saa 3.15 jana usiku baada ya gari aina ya lori kufeli breki na kuligonga kwa nyuma gari la aina ya Coaster lililokuwa na abiria 17 ambao wote walifariki hapohapo”, amesema Kamanda Kyando.

Kati yao abiria wengine wawili akiwemo dereva wamefariki wakiwa hospitali, lakini natoa wito kwa madereva wafuate sheria za barabarani hasa wanapofika maeneo yenye mwinuko mkubwa, na niwaombe ndugu wajitokeze kuitambua miili ya ndugu zao“, ameongeza Kamanda Kyando.

Kwa sasa miili ya watu hao 17 imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya uchunguzi.

(Visited 296 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us