ASSAs

VANESSA MDEE NA RAYVANNY WAPATA NAFASI YA KUTUMBUIZA TAMASHA LA ESSENCE MAREKANI

814
0
Share:

 wasanii wawili wa Bongo Fleva wametajwa kutumbuiza katika tamasha  kubwa la Essence
Festival nchini Marekani, wasanii hao ni Vanessa Mdee na Rayvanny.

Tamasha hilo ambalo kila mwaka hufanyika huko New Orleans, Louisiana mwaka huu limepangwa
kufanyika kuanzia July 4 hadi 7 mwaka huu.

Wasanii wengine wa Afrika waliotajwa kutumbuiza ni pamoja na Sauti Sol kutokea Kenya, Davido
kutokea Nigeria pamoja na Nasty C wa Afrika Kusini.

Wasanii wengine nje ya Afrika ni pamoja na Miss Elliot, Mary J.Blidge, Nas, H.E.R, Teyana
Taylor, Pharrell Williams na wengine.

Tamasha ya Essence fest lilianzishwa na jarida la Essence mwaka 1995 likiwa na lengo la kuwapa
nguvu wanawake wenye asili ya rangi nyeusi na kusherekea tamaduni na muziki wa watu wenye
asili ya Afrika nchini Marekani

(Visited 60 times, 1 visits today)
Share this post