ASSAs

KAMPUNI YA 361 DEGREES, TCCIA NA PKF East Afrika KUJA NA TUZO ZA KILIMO

916
0
Share:

Dar es Salaam

Kampuni inayojihusisha na masula ya masoko na Uhusiano wa umma 361 Degrees kwa kushirikiana na Chama cha wakulima wenye Viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA) na Kampuni PKF East Afrika wameandaa tuzo za kilimo ambazo zinafanyika Februari 12 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tuzo hizo kutoka kampuni ya 361 Degrees, Hurbert Kisasi amesema kuwa, tuzo hizo zimelenga kuwatambua wakulima pamoja na kuwatunuku vinara waliofanya vizri katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta hiyo.

Amesema kuwa, lengo la kuandaa tunzo hizo ni kuangalia ubunifu, ubora na kujitoa na wadau kwani sekta ya kilimo imekua ikichangia katika uchumi wa nchi huku ikiwa imetoa ajira zaidi ya asilimia 67 ya wananchi sawa na dola za kimarekani sh billion 13.9

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TCCIA, Fatuma Hamis amesema kuwa, kuna vipengele zaidi ya 40 ambavyo vitashindaniwa, hivyo amewataka wadau mbalimbali wa kilimo kuangalia kwenye mitandao ya kijamii na website za TCCIA ambapo mchakato wa tunzo hizo utaanza mach 6 hadi 27.

“TCCIA imefurahi kuwa sehemu ya utoaji wa tuzo hizi kwenye sekta ya kilimo na mnyororo mzima wa thamani, hii ni mara ya kwanza kutokea hapa nchini itawavutia watu wengi watakaosaidia kuikuza sekta hii ” amesema Fatuma.

Aidha, ametaja baadhi ya vipengele vitakavyoshindaniwa katika tuzo hizo ikiwa ni pamoja na mkulima bora wa mwaka, mbunifu katika kilimo biashara, mwanafunzi bora wa kilimo wa mwaka, matumizi mazuri ya teknolojia, tuzo ya vijana katika kilimo, mkulima chipukizi katika kilimo biashara pamoja na mbunifu wa kidigital wa mwaka.

Uchaguaji wa kutoa tuzo hizo katika vipengele vinavyoshindaniwa utaendeshwa na jopo la wataalam kutoka kampuni kubwa la Afrika Mashariki PKF inayojihusisha na masuala ya ukaguzi na ushauri wa biashara.

(Visited 71 times, 1 visits today)
Share this post