ASSAs

RAIS MAGUFULI ATOA HESHIMA YA MWISHO KWA MAREHEMU RUGE MUTAHABA

852
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mwasisi na mkurugezi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliyefariki dunia Februari 26, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa kipatiwa matibabu.

Rais Magufuli leo Machi 2, 2019 ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds media Group kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2,2019 katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam pamoja na kutoa

Pia  Rais Magufuli ametoa mkono wa pole kwa ndugu na familia ya Marehemu Ruge Mutahaba baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba  na kutoa pole kwa baadhi ya wananchi waliofika kwaajli ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Ruge Mutahaba.

Marehemu Ruge Mutahaba anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao siku ya Jumatatu Machi 4, Kiziru wilayani Bukoba mkoani Kagera na atasafirishwa kutokea Dar es Salaam siku ya Jumapili, Machi 3.

(Visited 75 times, 1 visits today)
Share this post