ASSAs

LADY JAY DEE AUNGANA NA WASANII WENGINE KUMSINDIKIZA RUGE KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

1033
0
Share:

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura ameshiriki na wasanii wengine leo wilayani Bukoba katika shughuli nzima ya kumsindikiza Mkurugenzi wa Vipindi Clouds media Ruge Mutahaba katika makazi yake ya milele.

Picha mbalimbali zimeonekana kurushwa katika mitandao ya kijamii akionekana akiwa katika uwanja wa ndege wa Bukoba pamoja na wasanii wengine akiwemo Linex pamoja na Mwana Fa.

Kumekuwa na maneno mengi yaliyokuwa yakiongelewa na watu katika mitandao ya kijamii kufatia ugomvi uliokuwa unasemakana upo kati ya wawili hao lakini Jay Dee ameonesha kuweka tofauti hizo pembeni na kushiriki ibada ya mwisho ya kumsindikiza Ruige Mutahaba katika makazi yake ya Milele.

(Visited 158 times, 1 visits today)
Share this post