ASSAs

BREAKING NEWS; MBOWE NA MATIKU WAACHIWA HURU KWA DHAMANA

899
0
Share:

Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko.

Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba.

 Uamuzi huo uliotolewa mapema leo Machi 7,2019 Jaji Sam Rumanyika  mahakamani umesema kuwa Mahakama imeikubali rufani hiyo kama ilivyo  hivyo warufani wanatakiwa wawe nje  na kwamba uamuzi wa kuwafutia dhamana ulifanyika mapema mno (pre mature).

“Aidha, sharti la kuripoti polisi kila alhamisi limefutwa badala yake watariporti mahakamani mara moja kwa mwezi si polisi tena kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kisutu mara ya kwanza,” amesema jaji Rumanyika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwafutiwa Mbowe na Matiko dhamana kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana hiyo ambapo walikata rufaa Mahakama Kuu Desemba mwaka jana na uamuzi kutolewa leo.

Walifutiwa dhamana hiyo na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri Novemba 23, 2018 lakini siku hiyohiyo kupitia kwa wakili wao Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura sana wakipinga uamuzi huo.

(Visited 69 times, 1 visits today)
Share this post