ASSAs

ILALA YATAMBUA MCHANGO WA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE

1792
0
Share:

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imewatambua mchango wa waandishi wa habari Wanawake sita katika kuitangaza Halmashauri hiyo na kufanikiwa kupata hati safi ya Mahesabu kwa Mwaka 2018/2019.

Hayo yalisemwa Dar es salaam Leo na Meya wa Halmashauri hiyo Charles Kuyeko katika hafla fupi ya kuwapongeza wandishi sita Wanawake.

Kuyeko alisema katika Manispaa hiyo ya Ilala Wanawake hao wamekuwa mstari wa mbele katika shughuli za Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Ilala katika kuandika TAARIFA mbalimbali za kijamii ,ikiwemo Afya, Mazingira,elimu .

“Kesho ni siku ya Wanawake Duniani Manispaa yangu imetambua utendaji kazi wa waandishi wa habari sita Wanawake Leo tumewatunuku vyeti vya shukrani kwa kutambua mchango wao wameifanya Halmashauri ya Ilala kupata hati safi ya mahesabu kwa miaka mitatu mfululizo “alisema Kuyeko.

Aidha alisema wana habari ni chombo chenye Heshima wataendelea kuheshimika katika Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Ilala inayoongozwa na Watendaji Wanawake kila idara.

Amewapongeza Watumishi wa Manispaa hiyo kwa mchango wao mkubwa katika utendaji wa kazi kwa kufanya kazi kwa weledi.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano Manispaa Ilala Tabu Shaibu, aliwataja waandishi hao Nora Damian Mtanzania, Futuna Seleman Itv, Beatrice Erick Chanel Ten, Cecy Jeremiah Uhuru FM, Lucy Ngowi Habari Leo na Eva Sekoko TBC1.

Tabu Shaibu alisema Nora Damian wa MTANZANIA ametambuliwa kupitia makala ya elimu aliyoiandika ambayo ilihusu changamoto za uhaba wa vyoo katika shule mbalimbali za halmashauri hiyo na makala hiyo imeiwezesha halmashauri kuja na mpango wa ujenzi wa choo maalumu cha mtoto wa kike.

“Nora alitoa makala bora ya sekta ya elimu kuielezea shule za Ilala kuzungumzia Choo cha Mtoto wa kike kumuwezesha mtoto wa kike hata anapokuwa katika hedhi kuweza kuhudhuria masomo bila shaka yoyote, hadi sasa halmashauri imeshajenga vyoo vitatu ni Halmashauri ya kwanza nchini kubuni Mpango endevu wa Kujenga vyoo shule zote “alisema Shaibu.

Shaibu alisema katika waandishi hao sita Wanawake Lucy Ngowi wa habari Leo amepewa tuzo Kwa TAARIFA za Mazingira.

Naye Mwandishi wa habari wa Chanel Ten Beatrice Erick alisema mchango wao chachu Manisipaa ya Ilala kwa kuitangaza ILALA katika taarifa mbalimbali za Halmashauri hiyo.

“Inafikia wakati urafiki unakuwa pembeni tunafanya kazi muda mwingine mazuri wakati mwingine mabaya “alisema Beatrice.

(Visited 247 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us