ASSAs

ANTU MANDOZA ANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE ETHIOPIA

1903
0
Share:

Mwanadada mwenye uraia wa Kitanzania ambaye ni Mjasiliamali, Mtangazaji na Msanii wa Filamu nchini  Antu mandoza  ameeleza mkasa mzima uliopelekea kunusurika katika ajali ya ndege ya shirika la  Ethiopia iliyotokea March 10,2019 asubuhi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mandoza ameeleza kuwa siku ya tukio hilo alitakiwa kusafiri na ndege ya shirika hilo aina ya Boeing 737 MAX ET302 ambapo aliamua kubadilisha ruti hiyo na ndipo aliposikia taarifa ya ajali hiyo hapo baadae.

Mandoza ameeleza hivi;

“@missmandoza I almost took the Ethiopian plane that crashed today I changed the route to Addis, I’m just landing and seeing the news and so many calls from the few people who knew I’m traveling with Ethiopia worried . God is good . Ningekua marehemu saivi🤭. Mungu mkubwa.”

Ikumbukwe kuwa ajali hiyo imeua watu 157 huku Taifa la Kenya likiwa limepoteza raia wake 32 na mpaka sasa taarifa zilizotolewa zimethibisha kuwa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyekuwepo ndani ya ndege hiyo.

(Visited 266 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us