ASSAs

ASUMPTER MSHAMA ATOA SOMO LA MALEZI KWA WANAWAKE WA KIBAHA

1072
0
Share:

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Asumpter Mshama amewataka wanawake wa mkoa wa Pwani kuwa na hofu ya Mungu kwa kuhakikisha wanatoa malezi yaliyo imara kwa watoto wao ili kuwalinda na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Mshama amezungumza hayo alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika Wilayani Kibaha ambapo alikaribishwa kama Mgeni Rasmi, amewataka wazazi kwa kushirikiana na serikali kuwakamata wazazi wa wawatoto ambao wameachichwa shule na hawaeleki mahala walipo.

“Kuna vitu vinafanyika vya kutrain(kufundisha) watoto wetu mambo yasiyo faa, jiulize watoto elfu tano mia sita kumi na mbili wavulana ni jeshi kubwa kuna mawaziri, madaktari kuna walimu wanaenda wapi? nilikuwa nataka tuliangalie kama mkoa kama tunakamata wazazi wa watoto ambao hawajaenda shule tukamate wazazi ambao hawajaendelea na shule watueleze wako wapi?” amesema Mshama.

Aidha amewaasa wanawake kutokukubari kutumia watoto katika mamboyasiyo faa, kwa kuhakikisha wanatoa malezi yaliyo bora na kutokukubari watoto kutumika kwa kuleta hasara.

Pia amewataka wanawae wajasiriamali wa Pwani kuboresha ufungaji wa bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya ufungaji, ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa bora na kupeleka bidhaa hizo kuwa zakimataifa zaidi.

Katika hatua nyingine Msahana amesema kuwa mpaka sasa Mkoa wa Pwani bado upo katika nafasi ya 10 katika maambukizi ya Ukimwi ambapo amewataka wamama na wakazi wa Pwani kuhakikisha wanabadili Tabia, kwa kuacha kufanya mambo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na kuacha vitendo vya uzinifu ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi.

“niwaombe wanawake tukikataa sisi na asilimia za ugonjwa wa ukimwi zitashuka wanaume watapona, hizi fedha tunazopata zitutoshe tukae na watoto wetu na kuongeza uchumi pasipo kuambukizwa ugonjwa wa Ukimwi” amesema Mshama.

 

(Visited 85 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us