ASSAs

WANAWAKE WA TAGLWU WALIA NA RUSHWA YA NGONO KAZINI

2232
0
Share:

Dar es Salaam

Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa Dar es Salaam wamesema rushwa ya ngono ni changamoto kubwa kwa baadhi ya Watumishi.

Kauli hiyo, ameitoa na Kaimu Katibu wa TAGLWU Mkoa Dar es Salaam leo Fatuma Kisangile wakati akisoma Taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ambaye alikuwa mgeni rasmi, katika sherehe za Wanawake wa Serikali za mitaa Tanzania TAGLWU Mkoa.

Fatuma amesema katika sehemu ya kazi rushwa ya ngono na matumizi mabaya ya madaraka ni tatizo ambapo baadhi ya Wanaume wenye madaraka ya juu hutumia nafasi zao kuwashawishi au kuwarubuni Watumishi Wanawake na kugeuza ngono ni kigezo cha mwanamke kupewa haki za Msingi za kiutumishi.

“Wanawake wa TAGLWU tunasema huu ni unyanyasaji mkubwa jambo hili halikubaliki tunakuomba Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ulibebe kwa kushirikiana na viongozi wenzako wa serikali muongeze nguvu kulikemea “alisema Fatuma.

Fatuma ameishauri Serikali iwawekee utaratibu wa siri wa kutoa taarifa ya matukio ya unyanyasaji Kijinsia (Sanduku la maoni)ili Watumishi wawe huru kutoa kero.

Aidha, amesema mara baada kuanzishwa kwa masanduku hayo Watumishi wa serikali watakaobainika kuwa na tabia hiyo wachukuliwe hatua kwani sisi Wanawake tunaona kama wapinga maendeleo.

Amesema kuwa, wote wenye tabia hiyo wachukuliwe hatua kwani wao wanaona kama wapinga maendeleo na wanakwenda kinyume cha sheria ya ajira mahusiano kazini ya mwaka 2004.

Ameongeza kuwa, changamoto ya Pili Wafanyakazi wanawake mahala pa kazi wanadharaurika hali hiyo inatokana na historia tangu awali ya mila na desturi kwamba Wanawake wanatumika kama chombo katika JAMII (mfumo dume)

Amesema wanawake wana uwezo mkubwa katika nyanja mbalimbali za uongozi hivyo ni muda muafaka kwa JAMII kubadili mtazamo wa mfumo dume ili tushirikiane kwa pamoia kuleta maendeleo na kulijenga Taifa.

Amesema kuwa, wafanyakazi kundi lingine bado lina changamoto ya madai yao Mbalimbali ya mda mrefu yanayotokana na likizo, uhamisho, matibabu,malimbikizo ya mshahara na madeni.

Fatuma alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mjema hafikishe katika mamlaka husika suala hilo ili waajili wao waweze kuwalipa haraka kwani Wapo wafanyakazi Wanawake wao ndio Tegemezi nyumbani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewagiza Makatibu Tawala wa kila wilaya kuwaruhusu watumishi hao waweke Sanduku la maoni ili serikali iweze kuchukua kero zao.

Pia Mjema amewataka TALGWU waunde kamati ya viongozi Wa Wajumbe wawe wanakutana na viongozi wa Wilayani kwa ajili ya kuwasilisha changamoto zao.

“Hongereni kwa umoja wenu huu kwa mara ya kwanza kunialika kuwa mgeni rasmi kwani aslimia 70 ya Wanawake mijini na vijijini ni wazalishaji wanajenga nchi hii ” amesema Mjema

(Visited 318 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us