ASSAs

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA MKOANI KIGOMA

768
0
Share:
Watu wa tatu wanaosadikika kuwa ni majambazi wameuawa Mkoani Kigoma na Jeshi la Polisi katika Operesheni ya kupambana na uhalifu iliyokuwa inafanywa na jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno, amedhibitisha kutokeo kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa Machi, 11 mwaka huu, polisi wake waliokoa mali zilizokuwa zimetekwa na majambazi hao ambapo walikuwa watano katika kutekeleza uhalifu huo.

Amesema majambazi hao walisimamisha gari aina ya ‘hiace pamoja na Landcruiser’ ila kulingana na uimara wa jeshi la polisi walifanikiwa kuokoa vitu hivyo.

Pamoja na hayo, Kamanda Otieno  ametoa onyo kali kwa wananchi watakaobainika kushirikiana na wahalifu mkoani humo.

Aidha amewataka  wananchi kufuata taratibu zilizowekwa na uhamiaji katika kuingiza nchini raia wa nchi jirani wanaotumika katika kazi za mashambani.

(Visited 40 times, 1 visits today)
Share this post