ASSAsSamaki Samaki

DC MAKORI AWAFUNDA VIKUNDI VYA WALEMAVU KIMARA

170
0
Share:

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori  amevitaka vikundi vya walemavu kuzitumia pesa walizopewa na Halmashauri kwa uadilifu mkubwa pamoja na nidhamu ili kufanikisha zoezi lililokusudiwa.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizindua zoezi la utoaji hundi kwa vikundi vya walemavu katika ukumbi wa kanisa la KKT Kimara, ambapk Manispaa hiyo, inatarajia kutoa jumla ya shilingi milioni 114 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu.

“Unaweza kuwa na wazo zuri ila usiwe na namna ya kuanza, ukisema utakopa bank itataka riba ila serikali imeweza kuliona hilo na kulitafutia ufumbuzi na ndio maana inatoa fedha za uwezeshaji”amesema Makori

Aliongeza kuwa, liko baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi taifa. Kwenye miongozo ya baraza lile kuna ambayo inaielekeza serikali kuwawezesha wananchi wake kiuchumi kutoka na wananchi kuipa dhamana serikali ya CCM ndio maana inatoa fedha za uwezeshaji kwa wananchi wake.

Katika hatua nyengine, Mkuu wa Wilaya alimshauri Mkurugenzi ashirikiane na wasaidizi wake kuanza kujipanga na kuhakikisha wanavilea vikundi hivyo vya walemavu.

“Leo tunawasema kama wafanyabiashara wadogo lakini wakisimamiwa vizuri na kufanya kazi zao ipasavyo, siku moja tutawaita mabilionea wa Tanzania”Aliongeza mkuu wa Wilaya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo bi. Beatrice Dominic alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuhudhuria na kuahidi kuendelea kutoa asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri kama utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Nae Mary Mgwai kwa niaba ya walemavu alishukuru serikali ya awamu ya tano kupitia kwa rais Mhe. John Pombe Magufuli, mkuu wa Wilaya Mhe. Kisare Makori na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Dominic. Aliwaomba waendelee kutoa mafunzo kwa vikundi vya walemavu ili fedha walizozipata ziweze kutumika kama ilivyokusudiwa.

(Visited 20 times, 1 visits today)
Share this post