lemutuz ASSAsSamaki Samaki

HUDUMA YA KUPANDIKIZA FIGO INAZIDI KUFANIKIWA NCHINI

49
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (Mb) mapema jana Machi 15,2019 ametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa na kuwapongeza timu ya madaktari wa Tanzania ambao jana walifanikisha kufanya  operesheni ya tano ya kupandikiza figo.

Wataalamu hao walifanya operesheni hiyo chini ya wasaidizi wataalamu kutoka nchini Japan.

 

 Dkt Ndugulile amewashukuru wataalamu hao kwa kuwajengea uwezo wataalamu wazalendo katika huduma za kibingwa.

Leo  wagonjwa wengine wawili watafanyiwa operesheni hiyo, Hadi hivi sasa, wagonjwa 43 wameshafanyiwa operesheni hii.

(Visited 13 times, 1 visits today)
Share this post

Leave a reply