ASSAs

JUKWAAA LA UWEZESHAJI WAOMBA MSAADA ILALA ENEO LA BIASHARA

1035
0
Share:

Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Kata ya Gongolamboto waiomba Manispaa ya Ilala wawapatie eneo la Biashara na kuwakutanisha Wajasiriamali mbalimbali.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Jukwaa Kata ya Gongo la Mboto Neema Mchau, wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Wanawake wa Kata hiyo.

“Sisi Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Wanawake kiuchumi Kata ya Gongolamboto mapendekezo yetu tunaomba Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ambaye mlezi wa Jukwaa mkoa utuombee eneo kwa Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Shauri kwa ajili ya kutumika kufanyia Biashara litakalowakutanisha Wajasiriamali wote wa Manispaa ya Ilala “alisema Neema.

Neema alisema dhumuni la kuwakutanisha Wanawake wote Wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala kwa mwezi mara mbili kuongeza ubunifu, ushindani na kujenga mahusiano.

Aidha alipendekeza wabuni fursa zikatazo wawezeshaji kupata vyanzo cha Mapato na kuinua mfuko wa Uwezeshaji wanawake Kiuchumi.

Akielezea historia ya Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake kiuchumi alisema Kitaifa lilizinduliwa Juni 2016. Na kuekekezwa majukwaa hayo yazinduliwe ngazi ya Mtaa dhumuni kuwafikia Wanawake wote kwani Wanawake ni kundi ambalo lipo nyuma katika shughuli za uzalishaji..

Akielezea Mafanikio alisema hivi karibuni walifanya ziara endelevu mpaka sasa wametoea elimu kwa Wanawake 573
Katika mitaa minne ya Kata hiyo.

Mafanikio mengine Kama kiongozi wa Wanawake wa Kata hiyo Vikundi 33 vimesajiliwa Halmashauri ya Ilala vikundi 18 vimepata mkopo na vikundi 15 vipo katika mchakato.

Kwa upande wake mgeni rasmi Mratibu wa Jukwaa Mkoa Dar es Salaam Dkt, Elzabeth Mshote ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alisema Serikali imeruhusu Kufanya biashara eneo la Viwanja vya Mnazi Mmoja majukwaa yote ya mkoa Dar es Salaam kutoka manispaa tano .

Mratibu Dkt.Elizabeth aliwataka kila alimshauri kuandika mikakati yake ya Biashara na kupeleka mapendekezo hayo mkoani,ili kuwapangia taratibu za ufanyaji Biashara eneo la Mnazi Mmoja ambapo kwa mwezi Biashara zitafanyika mara tatu.

Pia aliagiza maafisa Maendeleo wote Manispaa ya Ilala kuwafikia Wanawake wa jukwaa kwa wakati na kuwapa huduma katika maeneo yao ya kazi..

“Jukwaa la Uwezeshaji wanawake Kiuchumi sio jukwaa la siasa kwa ajili ya kutafuta fursa mpaka sasa kupitia Jukwaa Wanawake wengi wamejikwamua kiuchumi wanamiliki mamilioni”alisema Elizabeth.

Kwa upande mwengine aliwasimika Wanawake wa Kata ya Gongolamboto na kuwaeleza kuwa Uongozi ni dhamana viongozi wa Gongolamboto msimamie yote Kwa ajili ya Wanawake kwani Wanawake ni Jeshi kubwa.

Naye Naibu Meya Ilala Omary Kumbilamoto alisema Manispaa Ilala wametenga shilingi milioni 700 ya ajili ya kuwakopesha Wajasiriamali Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Kumbilamoto alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuwawekea utaratibu wanawake wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa Wilaya ya Ilala wakashiriki maonyesho mbali mbali nchini China.

Naye Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Georgis Asenga aliagiza Vikundi vyote vilivyoomba Mikopo Manispaa Ilala kufungua akaunti Benki ili waweze kupata mikopo kwa Wakati.

Asenga alisema Manispaa Ilala imeshatoa mikopo awamu ya kwanza kwa sasa halmashauri hiyo ipo katika mchakato wa kuandaa vikundi vya kuwapa mikopo ya serikali isiyo na riba awamu ya Pili Fedha zinazotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa Ilala.

(Visited 66 times, 1 visits today)
Share this post