ASSAs

SIMBA WAAHIDI KUANDIKA HISTORIA MPYA LEO TAIFA

957
0
Share:

Wachezaji wa Klabu ya Simba wameahidi kuwafurahisha mashabiki katika mchezo walionao leo dhidi ya timu ya AS Vita unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ietolewa na Nahodha wa timu ya Simba John Bocco jana katika mkutano alioufanya kabla ya mechi(Pre-Match Meeting), ambapo amesema wachezaji wotewapo vizuri na wamefanya mazoezi yakutosha na wako tayari kuandika historia nyingine ndani ya klabu hiyo.

”Tunaiheshimu AS Vita ni klabu yenye uzoefu katika michuano hii, lakini na sisi kama Simba ni klabu kubwa na tumejiandaa, tunataka kuweka historia jambo ambalo linawezekana” amesema Bocco.

Pia Bocco amaewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi  uwanjani na kuishangilia Simba kwani kwa kufanya hivyo watawapa nguvu zaidi nje ya uwanja na hatimaye kufanikiwa kushinda.

Simba inahitaji ushindi pekee leo ili iweze kusonga mbele kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutoka Kundi D, lenye timu za Al Ahly, AS Vita na JS Saoura.

 

(Visited 73 times, 1 visits today)
Share this post