ASSAsSamaki Samaki

WANANCHI WA KIBAMBA WALIA NA USAFIRI

155
0
Share:

Dar es Salaam

Wananchi wa kata ya Kibamba Wilaya ya Ubungo wameiomba Serikali kuwawekea vivuko katika mtaa wa Kiluvya ambacho kinaunganisha Madukani na kwa Komba eneo ya shule ya sekondari na msingi kiluvya kwani kipindi cha mvua wanafunzi wanapata shida sana pamoja na kivuko ambacho kinaunganisha Gogoni na Hondogo pia wanafunzi wanapata shida sana kipindi cha mvua.

Pia wananchi wamelalamikia kutokuwepo kwa kituo cha daladala eneo la kiluvya mwisho jambo ambalo linapelekea wanafunzi kupata shida ya usafiri sana kwani waategemea gari za kibaha, huku ikiw maeneo ya Kiluvya na Gogoni kuna shule nyingi za Serekali.

Wakizungumza na mtandao wa Lemutuz blog baadhi ya wanafunzi wa shule ya Kibamba;gogon,kiluvya sec wamesema changamoto hiyo imekua ya mda mrefu sasa ambapo hulazima kuchelewa kurudi nyumbani kwao na kutofanya vizuri katika mitihani yao kutokana na kutumia muda mwingi kukaa kituoni kwa ajili ya kusubiri usafiri.

Hamisi Ramadhani ni miongoni mwa wanafunzi wanaosoma shule ya Kibamba amesema kuwa, wanalazimika kulipa nauli 300 badala ya 200 ambayo ni nauli halali iliyopangwa na serikali kutokana na konda wa gari za abiria kuwazuia kupanda gari.

“Tunajitahidi kuwahi kufika kituoni ili tuweze kufika shule kwa lengo la kushiriki vipindi vya mwanzo lakini tunachelewa kufika kutokana na konda kutukatalia kuingia katika magari, tunapofika tumechoka sana hata tunashindwa kufanywa assegment zetu”amesema Ramadhani

Kwa upande wake, Konda wa Daladala ya Mlongazila Mbezi Joran David amesema kuwa ni kweli wanawatoza nauli wanafunzi 300 badala ya 200 na walimu 500 badala ya 400 kutokana na uhaba wa magari yaliopo yaliopo kwa sasa na ikilinganishwa na wingi wa wanafunzi.

Mtandao wa Lemutuz blog uliamua kufunga safari hadi kwa Diwani wa kata hiyo, Ernest Mgawe ili kuweza kutolea ufafanuzi wa suala hilo, ambapo amekiri ni kweli na yeye amekwisha toa malalamiko mara kadhaa katika mabalaza ya madiwani pamoja na ofsi ya mkuu wa wilaya lakini bado halijapatiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa, changamoto inayokwamisha kupatikana kwa eneo hilo la kituo cha daladala ni TANROADS ili SUMTRA waweze kutoa lesen za njia hiyo hadi kiluvya madukani ili Magari yaweze kufanya kazi na wanafunzi na wananchi waweze kuondokana na changamoto hiyo.

Hata hivyo amesema, amekua akifanya vizuri katika maeneo mengi ikiwa ni kusaidia wajane katika vipindi vya sikukuu ,na kuhakikisha vikundi kupata mikopo ya Manispaa zaidi ya 70 pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, hivyo ametekeleza ahadi zake kwa asilimia 85 alizowaahidi wananchi katika uchaguzi mkuu wa 2015, lakini Changamoto iliyopo kwa sasa ni kukosekana kwa ulinzi shiriki katika baadhi ya maeneo hali inayopelekea kuwepo kwa vitendo vya wizi.

Hussen Said ni miongoni mwa watu ambao waliokua viongozi wa ulinzi shiriki katika kata hiyo, lakini walishindwa kuendelea na zoezi hilo kutokana na kukosa ushirikiano kwa wananchi na baadhi ya watu kuwatishia maisha yao.

(Visited 20 times, 1 visits today)
Share this post