ASSAsSamaki Samaki

WILAYA YA UBUNGO SASA KUPATA 40% KATIKA VITEGA UCHUMI VYA OSTERBAY VILLA

205
0
Share:

Dar es Salaam

Manispaa ya Ubungo na Kinondoni wameingia mkataba wa makubaliano na mwekezaji wa osterbay Villa katika majengo mawili ambayo ni 322 RUVU RD na 277 MAWENZI RD zenye jumla ya apatiment 17 kila moja ikiwa na vyumba kuanzia vitatu na kuendelea.

Majengo hayo mawili ambayo ni vitega uchumi vya Manispaa hizo mbili yalikuwa yamefungwa kwa takribani miaka 8 pasipo kuingiza Mapato kutokana na kesi iliyokuwa mahakamani jambo ambalo ni hasara kubwa kwa Halmashauri za Manispaa zote mbili.

Kufuatia jitihada za wakuu wa Wilaya hizo mbili Mh. Kisare Makori wa Ubungo na Mh. Daniel chongoro wa Kinondoni walianza mazungumzo ya pamoja kuanzia jana tarehe 15/03/2019 na hatimaye jana kufikia muafaka wa kusaini mkataba na mwekezaji wa Osterbay Villa tayari sasa kwa majengo hayo kufanya biashara.

Vitega uchumi hivyo sasa vinaenda kuongeza mapato ya ndani ya Manispaa ya Ubungo katika asilimia 40 ambayo itasaidia kuboresha huduma za kijamii kama Afya, Elimu, miundo mbinu nk hivyo kuleta ustawi wa watu wetu.

Aidha kwa mujibu wa makubaliano ya mradi huo wa uwekezaji asilimia 60 ya mapato yatakuwa chini ya Manispaa ya Kinondoni na asilimia 40 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi Beatrice Dominic amesema anawashukuru sana wakuu wa Wilaya hizi mbili Ubungo na Kinondoni kwa kuwa jitihada zao binafsi zimeweza kuzaa matunda “nawashukuru sana”amesema Beatrice Dominic

(Visited 50 times, 1 visits today)
Share this post