ASSAs

MULTCHOICE TANZANIA YAJA KIVINGINE YATOA FURSA KWA WADAU WA SEKTA YA SANAA

285
0
Share:

Dar es Salaam

Mult Choice Tanzania leo March 19, 2019 wametoa fursa kwa wadau wa sekta ya Filamu iitwayo Talent Factory Portal ambayo itawasaidia wasanii kupanua wigo mpana wa kuuza kazi zao na kuweza kufanya biashara na watu ambao hawajawahi kukutana nao na kutengeneza kazi bora.

Katika uzinduzi huo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania amesema Fursa ya Talent Factory Portal ni fursa muhimu kwa wadau wa sanaa ambayo itawasaidia kupanua wigo wa kazi zao

“Fursa hii ya Talent Factory portal naiyona ni fursa muhimu Sana kwa wadau wa sekta ya Fulamu kwasababu inawapa wigo mpana wa kutengeneza mtandao wa kuuza kazi zao, kuweza kujifunza kutoka kwa wenzao na kujitathimi wapo kwenye kitengo gani kwenye tasnia ya Filamu”

Aidha amesema kuwa fursa hiyo ya Talent Factory Portal ni fursa ambayo inaweza kutuondoa kutoka dunia ya sasa na kutupeleka kwenye dunia ya kidigitali ambapo itasaidia kufanya biashara na watu ambao hawajawahi kukutana nao na kufanya kazi bora

“Talent Factory Portal ni fursa ambayo inatuondoa kutoka dunia ya sasa na kutupeleka kwenye dunia ya kidigitali, inatukumbusha kwamba tusiwe tunatumia mitandao kwaajili ya kuangalia instagram nani kaposti bali, kufanya biashara na watu ambao hatujawahi kukutana nao na kutengeneza kazi bora”

Mbali na hayo Joyce Fissoo amemaliza kwa kuwaomba wadau wawe wanajitokeza kunapotangazwa fursa Kama hizo kwasababu fursa hizo ndo mwokozi mkubwa katika dunia ya sasa ya teknolojia ili kuweza kuuza kazi zao na kukuza pato lao na kukuza pato la Taifa kwa ujumla

(Visited 16 times, 1 visits today)
Share this post