ASSAs

PROF LIPUMBA AWAANGUKIA WAZANZIBAR, AONDOA KINYONGO KWA WAFUASI WA MAALIM SEIF

807
0
Share:

Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa yupo tayari kufanya kazi na wanachama wote waliokua wanamuunga mkono aliyekua Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Shariff.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni muda mchache baada ya aliyekua Katibu Mkuu wa Chama hicho kukabidhiwa kadi namba moja ya ACT Wazalendo na kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe.

Aidha ameowamba wanachama wa CUF walioko visiwani Zanzibar kuacha kuharibu rasilimali za chama hicho, huku akiwasihi kukiunga mkono chama chao na kushirikiana pamoja katika kujega CUF .

“Tupo tayari kufanya kazi na wale wote waliokuwa wakimuunga mkono maalimu seif watakaokuwa tayari kuendelea kubaki katika chama na kuachana na mgogoro uliokuwepo na kuanza kufanya shughuli za kuijenga jamii kwa kupigania haki ” amesema Prof Lipumba.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Khalifa Suleiman Khalifa, amesema kuwa kitendo kinachofanywa sasa kuendelea kuchoma bendera na kubadilisha ofisi za chama cha CUF ni makosa makubwa na hakutawasaidia kitu wale wote wanaofanya hivyo.

“Kitendo kinachoendelea sasa hivi visiwani Zanzibar kwa wanachama wanaomuunga mkono maalim seif kuharibu mali za chama hawatofaidika na lolote kutokana na orodha ya mali hizo kufikishwa kwa msajili wa vyama vya siasa ” amesema Khalifa

Naye,Mbunge wa Jimbo la Mchinga (CUF) Mkoani Lindi Hamidu Bobali aliyekuwa upande wa Maalimu seif amesema ndani ya miaka mitatu chama chao kilikuwa kama jehannam pahala penye giza nene na hawakujua kesho wala jana yao kutokana na migogoro ilikuepo ya kukwamisha harakati za kujenga chama.

“Sasa ni wakati wa kukijenga chama na kazi inze kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa tuwaonyeshe kuwa CUF ndicho chama kinachobeba ajenda za wananchi nilikuwa upande usio sahihi upande wa maalim lakini sasa nimerudi Nyumbani”amesema Bobali

Ameongeza kuwa haoni haja ya kuhama chama kutokana na mahakama kutoa uamuzi ambao walikuwa wakiusubiria kwa muda mrefu hivyo ni bora kuendelea kuongeza juhudi kuwapigania wananchi na si kupambana wao kwa wao.

(Visited 114 times, 1 visits today)
Share this post