ASSAs

ASILIMIA 70 ZA AJIRA ZATAJWA KUTOKA SEKTA BINAFSI

693
0
Share:

Imebainishwa kuwa asilimia 70 za ajira zinazotolewa nchini Tanzania zinatolewa na sekta binafsi ambapo pia imeelezwa kuwa sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuiwezesha nchi kufikia malengo endelevu kutokana na shughuli zake ambazo zimekua zikishughulikia ni pamoja na mazingira, sekta ya elimu na Maendeleo ya uchumi kiujumla.

Akizungumza na waandishi mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano uliokutanisha mashirika pamoja na asasi za kiraia lengo likiwa ni kupata maoni ya maendeleo endelevu kwa kujumuisha na umoja wa mataifa, Mwenyekiti wa bodi Umoja wa hiali nchini ya umoja wa mataifa (UN GLOBA COMPAT) Simon Shayo amesema kuwa, sekta binafsi ina mchango kuiwezesha nchi kuweza kufikia katika maendeleo endelevu.

Shayo amesema kuwa mpaka hivi sasa zipo  fursa mbalimbali ambazo kama sekta binafsi zitaendelea kuzitumia vizuri basi ni lazima nchi itapiga hatua kubwa zaidi, amesema maendeleo mengi yanayopatikana katika uchumi yamekuwa yakiguswa sana na sekta binfsi, ambapo amesema kuwa mpka hivi sasa Sekta hizo binafsi zimeweza kusaidia katika kuleta maendeleo ya watu kwa asilimia kubwa.

“Maendeleo endelevu yana lengo la kuwavuta wadau wote wa jukwaa la sekta binafsi na maendeleo ya kiraia, tukiangalia ajira nyingi tu za nchi hii tunaona zaidi ya 70% zinatokea ndani ya sekta binafsi hata miundombinu inayojengwa ni lazima tuiunganishe na sekta binafsi ili kupunguza umaskini nchini” Amesema Shayo.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini (UN) Alvaro Rodriguez, amesema kuwa katika malengo 17 wanayoyajidili yapo malengo muhimu ambayo kama nchi ikiwekea mkazo na kuyashinda basi nchi itafanikiwa kutoka katika tatizo la umaskini.

Rodriguez ameainisha maeneo hayo kuwa ni pamoja na uwkezaji wa viwanda nchini, mabadiliko ya tabia ya nchi ,pamoja na upande wa elimu, amesma endapo tatizo la ubaguzi wa kijinsia katika utoaji wa elimu utadhibitiwa vya kutosha basi itasaidia kuepuka tatizo la ajira nchini.

Naye Mwenyekiti wa Sekta binafsi TPSF Godfrey Simbeye amesema kuwa mipango yote 17 ya maendeleo endelevu yapo katika dira ya maendeleo endelevu ya mwaka 2025, amesema  mpaka hivi sasa kwa asilimia 45 ya vituo vya afya vinamilikiwa na sekta binafsi.

Amesema kuwa mpaka sasa ni asilimia 95 ya wafanyakazi walioajiliwa ajira rasmi wapo ndani ya sekta binafsi, ameeleza kuwa ili kuangalia fursa za kukaribisha watu kuwekeza nchini basi ni lazima watengeneze mazingira mazuri, pia amesema kwa sasa Sekta binafsi anashirikiana na serikali ili kuhakikisha kwa pamoja wanaleta maendeleo.

“Tunasema sekta binafsi inahusika sana katika maendeleo ya watu kwasababu tukianza kuangalia viwanda vingi ambavyo tunavyo nchini vingi vipo katika Sekta binafsi hivyo vinashiriki sana katika utoaji wa ajira kwa watu, tena mpaka sasa ni asilimia  95% ya ajira zilizo rasmi zinatoka sekta binafsi, kwa hiyo mbali na kuchangia kodi lakini pia tunaleta maendeleo katika nchi yetu.

Pia tunataka kusema hivi nchi kama Tanzania tuache kujivunia kila siku kwenye mikutano tunasema tuna fursa nyingi tuna madini,tuna gesi tuvichukue hivi vitu alafu tuviweke katika fursa watu waweze kuwekeza sasa, kwa maana hata wakati maendeleo endelevu yanaanzishwa sekta binafsi ilihusishwa sana kwa hiyo mpaka sasa Tanzania hatujaachwa nyuma katika maendeleo ya sekta binafsi” Amesema SAimbeye.

Aidha Simbeye amesema kuwa majadiliano hayo ya maendeleo endelevu ni lazima pia yafike kwa wananchi waishio vijijini ili kutoa fursa pia ya wananchi hao kujadili ili kuweza kutanua wigo wa maendeleo ya sekta binafsi na nchi kwa ujumla na sio kuishia mjini tu.

 

 

(Visited 46 times, 1 visits today)
Share this post