ASSAs

MCHUMBA WA BEN POL AGOMA KUITWA MAMA

1852
0
Share:

Mchumba wa msanii wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ anayejulikana kwa jina la Anerlisa Muigai amegoma kuitwa mama kwa sasa hivi, ambapo amefunguka na kusema hayupo tayari kwa sasa.

Katika mahojiano yake na mitandao ya Kenya, Anerlisa ambaye ni mjasiriamali mkubwa nchini humo akiwa anamiliki Kampuni inayohusika na maji ya kunywa alisema kuwa, licha ya kupenda sana watoto, lakini linapokuja suala la kubeba ujauzito anaogopa na hayupo tayari kwa sasa.

Mimi ni mmojawapo kati ya watu wanaopenda sana kuwabeba watoto wa rafiki zangu na kucheza nao. Binafsi sijawahi kabisa kufikiria kuja kuwa mama labda taratibu huko mbeleni nitakuja kwa sababu mchumba wangu ameniambia kuwa ndoto yake ni kupata mtoto wa kike,” amesema Anerlisa.

Wawili hao waliingia rasmi kwenye uhusiano April, mwaka jana ambapo mwishoni mwa mwaka walitangaza rasmi kuwa pamoja. Tayari ndugu wa pande zote wameshakutana Nairobi, Kenya na kinachosubiriwa ni ndoa.

(Visited 238 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us