ASSAs

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

1275
0
Share:

PMO_0526

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald Billet (kulia) wakifungua  kiwanda cha kuchakata muhogo cha CSTC kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye  Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.

PMO_0561

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuwasha mashine ya kuchakata muhogo wakati alipozindua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na wa pili kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick   Clavier.

PMO_0559

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuwasha mashine ya kuchakata muhogo wakati alipozindua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoni Lindi, Machi 22, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na wa tatu kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick   Clavier.

PMO_0565

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya uchakataji muhogo wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata mhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.

PMO_0613

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi Machi 22, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah, Naibu Waziri wa kilimo, Omari Mgumba, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Mwenyekiti wa CSTC, Gerald Billet, Balozi wa ufaransa nchini, Frederick Clavier, Mkurugenzi Mtendaji wa CSTC, Christophe Gallean na kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye

PMO_0659

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfuko wenye unga wa muhogo wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kwenye kijiji cha Mbalala katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah.  Kulia kwa Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga na kushoto ni Shift Leader wa CSTC, Samwel Ponera

PMO_0687

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limkited (CSTC) baada ya kukifungua kwenye kijiji cha Mbalala katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashra, Joseph Kakunda na wa pili kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga.

PMO_0736

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzani Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.  Wa tatu kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick Clavier, wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CSTS, Christophe Gallean. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

………………………..

*Awataka wakulima kuchangamkia fursa kwa kulima kwa wingi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara watumie fursa ya uwepo wa kiwanda cha kuchakata muhogo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi kwa kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kujiongezea kipato.

“Kama unataka pesa nenda kalime muhogo kwani kuna soko la uhakika na pia zao hili ni la muda mfupi na kilimo chake ni rahisi. Kwa sasa hatuna muda wa kukaa vijiweni vijana jiungeni katika makundi na muanzishe mashamba ya mihogo soko lipo tena mwenye kiwanda atawafuata hukohuko shambani.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 22, 2019) wakati akifungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi.

Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli la kuhamasisha ujenzi wa viwanda ni kusaidia katika kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini kabla ya kuuzwa.” Mbali na kuongeza tija kwa wakulima pia viwanda vinatoa ajira nyingi”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amekipongeza kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara kwa kazi nzuri ya utafiti wa mbegu za mazao mbalimbali wanayoifanya. Amesema kituo hicho ndicho kilichotafiti mbegu bora za muhogo zenye uwezo wa kuzalisha tani 20 hadi 50 kwa hekta.

Kwa upande wake, Balozi wa ufaransa nchini, Balozi Frederic Clavier amesema Serikali ya Ufaransa ipo tayari kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika mkakati wake wa kukuza uchumi hadi kufikia uchumi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni ushuhuda tosha wa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa na kilimo ni miongoni mwa mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania.

Nae, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewashukuru wawekezaji hao kwa uamuzi wao wa kujenga kiwanda cha kuchakata muhogo nchini kwa kuwa wamewezesha wakulima wa zao hilo kupata soko la uhakika na vijana wengi kupata ajira.

Kwa upande wake,Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msukumo alioutoa wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini kwa kuwa umechangia kuboresha maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

Mbunge huyo amesema uwekezaji katika sekta ya viwanda umesaidia kupunguza changamoto ya ajira hususani kwa vijana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa juhudi zake, kwani hatukutarajia kuwa na kiwanda katika eneo hili”.

Awali,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CSTC, Christophe Gallean alisema kiwanda hicho ambacho kilianza kujengwa mwaka 2012 kinazalisha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu cha ubora na kinauza unga huo katika nchi za Afrika Mashariki, Kusini, Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani.

Alisema kiwanda hicho chenye wafanyakazi zaidi ya 420 ambapo Watanzania ni asilimia 97 kina uwezo wa kuchakata tani 60 za muhogo mbichi kwa siku, ambao ni sawa na tani 25 za unga bora wa muhogo kwa siku.

(Visited 97 times, 1 visits today)
Share this post