ASSAs

KAIMU MEYA ILALA AMPA SIKU 14 MKUU WA KITUO KIDOGO CHA POLISI VINGUNGUTI

753
0
Share:

Dar es Salaam

Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala ambae pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto amempa siku 14 mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Vingunguti Inspecta Amani Mlimuka kuhakikisha amelitatua tatizo la skari vidole.

Agizo hilo limekuja mara baada ya Diwani huyo kupokea malalamiko mengi kwa wakaazi wa Vingunguti kuchoshwa na tabia za askari vidole kuwabambikizia kesi kwa kile kinachodaiwa ni wazembe na wazururaji.

Amesema kuwa, wananchi wa kata hiyo wamekua wakiishi kwa hofu kubwa kutokana na askari hao kutembelea na pingu kwa ajili ya kuwakamata vijana ambao hawana kazi huku wakiwabamkizia kesi na kumalizana bila kufika kituo cha polisi.

“Asilimia kubwa ya wananchi wa kata hii hawana kazi, lakini kumekua na tabia ya uonevu mkubwa, wakachukuliwa pesa zao, wanapewa kesi ambazo sio zao,hili ni tatizo nakuomba Insp Amani ulimalize tumechoka kama utashindwa nitakwenda ngazi za juu ” amesema Kumbilamoto.

Diwani Kumbilamoto akihutubia katika mkutano wa kutatua changamoto za askari vidole Vingunguti 

Aidha, amewatahadharisha wananchi watakaoshiriki katika ujenzi wa Machinjio ya kisasa ya kimataifa itakayojengwa Vingunguti ambayo inagharimu sh bill 12 kutoiba vifaa vyovyote vya ujenzi huo kwani watajikuta wanamalizia maisha yao gerezani.

Kwa upande wake, Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Vingunguti Inspecta Amani Mlimuka amesema kuwa yeye lengo lake ni kuhakikisha analinda amani, raia na mali zao hivyo hayupo tayari kuchafuliwa kwa sababu

Amesema kuwa,amekua akishirikiana na askari vidole pale tu anapowahitaji kwa ajili ya kazi maalum hivyo kama kuna mtu yoyote anaefanya vitendo vya kihalifu kwa wananchi kwa kutumia mgongo wa polisi basi atakula nae sahani moja.

“Hawa askari wagambo wamepewa maelekezo na Mkuu wa Mkoa ambapo wanapatikana ofisi ya mtendaji, hivyo kama kweli Philoteus Christopher Mpangala unajihusisha na masuala ya uhalifu na unyanyanyi naomba ujirekebishe nitakuchukulia hatua ” amesema Inspecta Amani

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo, mtaa wa Miembeni Suleiman Mohamed Said amesema kuwa, wamekua wakifanyiwa vitendo vya kihalifu lakini kesi nyingi hazifiki kituoni kutokana na askari vidole kuwabambikizia kesi na kumalizana vichochoroni.

Amesema kuwa, kuna gari ya askari kutoka buguruni ambayo inakwenda mitaa ya relini ikiwa na askari wasiopungua 6 kwa lengo la kwenda kudai pesa kwa wafanyabiashara waliopo maeneo hayo na anaekataa kutoa pesa hizo wanawabambikizia kesi

(Visited 36 times, 1 visits today)
Share this post