ASSAs

KUMBILAMOTO AFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MTENDAJI WA KATA LIWITI

1276
0
Share:

Dar es Salaam

Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala ambae pia ni Diwani  Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto,amesema kuwa watendaji wengi wamekuwa chanzo cha kukwamisha miradi ya maendeleo badala yake viongozi wa ngazi za juu kutupiwa lawama kutokana na uzembe wanaoufanya wa kushindwa kusimamia ujenzi wa miradi.

Aidha, ametoa agizo kwa Afisa mtendaji wa kata Remmy Misheck kuhakikisha pesa zote zilizoombwa katika mfuko wa jimbo kwa ajili ya kujengea matundu ya vyoo na kujengea madarasa zirudishwe katika mfuko wa jimbo kutokana na kushindwa kutekeleza miradi hiyo.

Hatua hiyo imejiri mapema leo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika shule ya msingi Liwiti na kimanga na kubaini kuwa fedha zilizotolewa katika mfuko wa jimbo hazijafanyiwa kazi tangu mwezi wa Januari zilipotolewa hadi leo hali inayopelekea wanafunzi wa shule hizo kupata usumbufu wa madarasa na matundu ya vyoo.

Amesema kuwa, mfuko wa jimbo ulitoa shilling mill 34 kwa ajili ya kuvunja vyumba viwili vya madara na kuyajenga mapya shule Liwiti na shilling mill 10 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo katika shule ya Tmdingi Tumaini Tabata kimanga ambapo pesa zote hizo hazijafanyiwa kazi yoyote

“Pesa ziliombwa na kamati za shule katika mfuko Jimbo zimeshaingizwa katika akaunti ya kata iweje mpaka sasa Ujenzi haufanyiki, tunataka kuona matokeo tunatakiwa kumsaidia Rais wetu kuhakikisha miradi yote iliyotengewa fedha inakamilika mwalimu mkuu kutana na Injinia ukabidhiwe mchoro na BOQ ujenzi uanze haraka sana” amesema Kumbilamoto.

Aidha amemuagiza Afisa Utumishi wa Manispaa Ilala Benivikta Mwaikambo kumuhamisha mtendaji wa kata ya Liwiti Remmy Meshack kutokana na uzembe alioufanya huku akiitaka Idara ya uchumi kupeleka pesa kwa waliohitaji.

Amesema kuwa, haoni sababu za msingi kwa watendaji hao kuendelea kuzishikilia pesa hizo katika akaunti huku wakijua wanafunzi wanateseka kwa kukosa madarasa ya kusomea na matundu ya vyoo wakati mfuko wa jimbo umeshatoa pesa hizo kwa ajili ya kutatua changamoto hizo.

“Lengo la watendaji hawa ni kutaka kumchafua Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah kwa wananchi wake kutokana na sababu wanazozijua wao,  ila mimi kama Kaimu Meya siwezi kulifumbia macho hili kwani hata Rais wetu Dk Magufuli linamtia doa”amesema Kumbilamoto

(Visited 337 times, 1 visits today)
Share this post