ASSAs

YANGA SC KAMILI KUIFUTA NDANDA FC KESHO

598
0
Share:
Jumla ya nyota 20 wa kikosi cha mabingwa wa kihistoria nchini, Yanga 
Sc, kesho alfajiri kitaanza safari kueleka Mtwara tayari kwa mchezo wa 
ligi dhidi ya wenyeji Ndanda Fc, mchezo uliopangwa kutimua vumbi, April 
4 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Afisa habari Dismas Ten ameiambia Yanga Tv mapema leo kuwa Nahodha 
Ibrahim Ajib ataendelea kukosekana kikosini kupisha majeraha madogo 
aliyo nayo huku Juma abdul akirejea kikosini baada ya kupona majeraha 
yake.
“Ibrahim Ajib bado tutaendelea kumkosa kikosini kutokana na majeraha ya 
mguu,lakinijambo jema ni kwamba Juma Abdul amerejea kikosini na atakuwa 
sehemu ya msafara wa kikosi chetu,mchezo utakuwa mgumu lakini maandalizi 
tuliyoyafanya yanatosha kutupa matokeo mazuri”.
 
Zaidi ingia www.yangasc.co.tz
(Visited 43 times, 1 visits today)
Share this post