ASSAs

MAKAMU WA RAIS ALIVYOFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA KUMBUKUMBU YA HAYATI ABEID AMANI KARUME

904
0
Share:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 
Mjane wa Marehemu Bibi Fatma Karume akizungumzia namna walivyohamasisha wanawake wapewe fursa ya kupiga kura kwenye harakati za kutafuta Uhuru wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Hayati Mzee Karume ni kielelezo cha misingi ya falsafa za Uwazi, Uadilifu, Ushirikishwaji, Upendo , Amani na Ubunifu ambazo ni Tunu alizoishi nazo kipindi cha maisha yake ya ujenzi wa Taifa la Zanzibar.Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. 
Hayati Mzee Karume alifanikiwa kuweka misingi ya utendaji wenye kuacha alama katika maisha na mifumo mbalimbali ya Kiserikali ambapo katika kipindi chake cha Uongozi alifanya mambo mengi ambayo hadi leo hii yamebaki kuwa kielelezo cha uongozi wake.
tutumie muda huu kutafakari hekima, busara na falsafa za Mzee Karume kwa maendeleo na mustakabali wa Zanzibar na Wananchi wake”alisema Makamu wa Rais
 
Aidha, Makamu wa Rais amewataka Viongozi wa sasa kujifunza kutoka kwa viongozi waasisi wa Taifa hili kwani wao walijitolea kutumikia wananchi kwa kuzingatia haki na usawa.
Mwaka huu tunaadhimisha miaka 47 tangia Mzee wetu atangulie mbele za haki Viongozi wa Zanzibar hatuna budi kujitafakari na kujitathmini kwa kina kama tunayofanya ni ndio au siyo”alisisitiza Makamu wa Rais.Makamu wa Rais alimuelezea Hayati Mzee Abeid Karume alipinga rushwa, ubadhilifu, alikuwa hapendi uzushi na uongo, alikuwa muwajibikaji na aliyezingatia Ilani ya Afro Shiraz na kusimamia yale waliyojiwekea kwa maendeleo ya Zanzibar.Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Ndugu Stephen Wasira amesema Chuo hiko ni chuo pekee kinachofanya kazi ya kuyaenzi mazuri yaliofanywa na waasisi wa nchi hii na kuwafundisha Viongozi na Vijana.
Vilevile Bibi Fatuma Karume alitumia nafasi yake ya kusalimia walihudhuria Kongamano hilo ambapo pamoja na kuwapongeza lakini aliwataka Wanawake kuendelea na mshikamano katika kujenga nan chi huku akitolea mfano namna yeye alivyopigania haki ya wanawake kupiga kura na leo anayo furaha kushuhudia mwanamke kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(Visited 64 times, 1 visits today)
Share this post