ASSAs

WAZIRI LUGOLA AMPA MWEZI MMOJA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI KUWASAKA MADALALI WA WAHAMIAJI HARAMU NCHINI NA NJE YA NCHI

1516
0
Share:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wakujadili masuala ya Wahamiaji haramu katika nchi hizo. Lugola alimpa mwezi mmoja Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), awasake popote walipo madalali wa wahamiaji haramu waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka nchini. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo. 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), Dk. Anna Makakala, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wakujadili masuala ya Wahamiaji haramu katika nchi hizo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Waziri wa Nchi, Wizara ya Amani Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia, Zeynu Jemal, wakati walipokuwa wanatoka katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wa kujadili masuala ya Wahamiaji haramu ndani ya nchi hizo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kenya, Michael Oyugi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wakujadili masuala ya Wahamiaji haramu katika nchi hizo. Lugola alimpa mwezi mmoja Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), awasake popote walipo madalali wa wahamiaji haramu waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka nchini. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (katikati-waliokaa), Waziri wa Nchi, Wizara ya Amani Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia, Zeynu Jemal (watatu kulia waliokaa), Mkurugenzi wa Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kenya, Michael Oyugi (watatu kushoto waliokaa), na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala, wakiwa katika picha na wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Ethiopia, mara baada ya kumaliza Mkutano wa Kimataifa wa Nchi hizo uliojadili masuala ya Wahamiaji haramu. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amempa mwezi mmoja Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), awasake popote walipo madalali wa wahamiaji haramu waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.Lugola alisema lengo la agizo hilo ni kuvunja mtandao mkubwa wa wahamiaji haramu nchini ambao kila mara wanakamatwa lakini bado wahamiaji hao haramu wanazidi kuongezeka.Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, leo, ambao ulikuwa unalenga kuweka mikakati ya kupambana na tatizo la wahamiaji haramu ndani ya nchi hizo, Lugola alisema tatizo hilo ni kubwa Tanzania, Afrika na dunia hivyo lazima wahakikishe wanaliondoa.Lugola alisema chanzo kikubwa cha tatizo hilo ni kutokana na uwepo wa madalali wa wahamiaji haramu ambao wanafanikisha wahamiaji hao wanasafirishwa kwa wingi katika nchi hizo wakiwahifadhi na kuwasaidia kwenda maeneo ambayo wamepanga kusafiri.
Mkutano huu ni mkubwa ambapo umeshirikisha nchi tatu ambapo mawaziri wake tupo nao, mkutano huu ni wa juu, ulitanguliwa na mkutano wa wataalamu ambao ulifanyika kwa siku mbili na walifanikiwa kutuletea mapendekezo yao,” alisema Lugola.Alisema baadhi ya mapendezo ya wataalam hao, ni pamoja na kupambana na biashara hiyo ya wahamiaji haramu, kuona umuhimu wa wahamiaji haramu kutopelekwa mahakanani na kuwafunga magerezani.
Idadi kubwa ya wahamiaji haramu hapa nchini ni Waethiopia, hivyo wataalam wa mkutano huu walipendekeza kuwepo na mawazo mbadala ambapo wahamiaji hao haramu wanapokamatwa nchini ndani ya siku chache tunawarudisha walipotoka, ambapo Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wahamiaji (IOM) watasaidia kuwasafirisha katika nchi wanazotoka,” alisema Lugola.
 
Alisema tatizo la kuwasaka madalali hao si kwa Tanzania tu bali ni kwa nchi zote tatu ambazo watawasaka madalali hao kwa nguvu zote mpaka wahakikishe tatizo hilo limemalizika au kupungua kwa kiasi kikubwa.
 
“Kuwasaka hawa madalali, sio tu kwa nchi zetu hizi tatu, bali tutawasaka kwa kasi zote mpaka Afrika Kusini, lengo letu kuu ni kuvunja mtandao huu, na kutokana na hilo naomba kuwaonya baadhi ya Watanzania ambao wanawapokea wahamiaji haramu, kuwapa chakula, kuwaficha na kuwahifadhi katika jengo lolote, wenye tabia hiyo nao tutawakamata” alisema Lugola.
 
Lugola pia alisema licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa za utendaji kazi kutokana na kuwa na ukosefu wa vifaa, aliwapongeza maafisa uhamiaji katika mikoa mbalimbali nchini kwa kuendelea kufanya kazi nzuri, lakini aliwataka waongeze kasi ya kulinda mipaka usiku na mchana kwa kuwakamata wahamiaji haramu mpaka mtandao huo umalizike.
(Visited 145 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us