ASSAs

TAKWIMU ZA TP MAZEMBE KUIHAMASISHA SIMBA SC

1151
0
Share:

Tp Mazembe wamepoteza michezo minne kwenye ligi ya kongo mpaka sasa. Mechi ya mwisho wa ligi walipoteza dhidi ya Saint Eloi Lupopo goli moja wakiwa kwenye dimba lao la Stade TP Mazembe uliopo Lubumbashi.

Simba wao wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi ya Tanzania (TPL). Mchezo wa mwisho simba walishinda goli 3 bila dhidi ya Mbao Fc.

TP Mazembe ambao ni mabingwa mara tano(5) wa klabu bingwa Afrika wanaimani wachezaji wao wakuyegemewa Tresor Mputu na Ben Malango watakuwa tayari kuivaa Simba siku ya Jumamosi, matumaini makubwa nikwamba walishaanza kufanya mazoezi na timu na mpaka sasa wapo Tanzania.

TP Mazembe kwenye hatua ya Makundi walifanikiwa kufunga jumla ya magoli 13 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara nne(4) tu. Simba wa wakiwa wamefunga magoli sita(6) na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara kumi na tatu (13) kwenye klabu bingwa.

Kwa baadhi ya takwimu hizi kwenye klabu bingwa hatua ya Makundi Simba ataweza hatua hii inayo hitaji zaidi magoli mengi dhidi ya mpinzani wako na kutoruhusu nyavu zako zisitikiswe?

(Visited 79 times, 1 visits today)
Share this post