ASSAs

MATIKO AMSHUKURU JAJI RUMANYIKA

2125
0
Share:

Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ametoa shukrani kwa Jaji Rumanyika kwa kuwapatia chamana, pia amesema kuwa kwenda kwake gerezani yeye ni neema.

Matiko ameeleza hayo alipokuwa katika mkutano wa hadhara mkoani Tarime, amesema anaamini wao kukaa Rumande kwa takribani miezi 3 ilikuwa ni mipango.

Wote tunajua masharti ya dhamana, kuna Mahakimu wengine wanaendeshwa. Hakimu Mashauri namtaja bila kuogopa na amebakisha mwaka mmoja kustaafu lakini sasa hivi amekuwa Jaji, ila namshukuru Jaji Rumanyika alieleza hukumu yake na kuweka mwanzo mzuri kwa Watanzania.” amesema Matiko

Kwa upande mwingine ilikuwa ni neema kwangu, mimi nilivyoenda Segerea nimeona mengi, kwa hiyo nitaendelea kuwatetea watanzania wengine, japo kwa sasa CCM wameanza kupiga propaganda eti nataka kuhamia Kinondoni“, ameongeza Matiko.

Ikumbukwe kuwa Mbowe na Matiko walikaa rumande kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa  na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba, 2018.

(Visited 266 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us