ASSAs

BODI YA FILAMU WAANDAA KONGAMANO KUSAIDIA WASANII NCHINI

1957
0
Share:

Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha waingizaji Taifa(TDFAA) wameandaa kongamano la waingizaji litakalofanyika Aprili 15, mwaka huu katika ukumbi wa SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya ‘Tujitambue, Tujithamini, Tujitangaze’ litakuwa na lengo la kuwajengea uwezo waigizaji katika maeneo yao kujitangaza ili kuleta ubora katika kazi zao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alisema kuwa Bodi hiyo imekuwa ikiendesha warsha mbalimbali ikiwemo umuhimu na uweledi na taaluma katika filamu.

Fissoo alisema kupitia kongamano hilo, wameadhimia kukutana na waingizaji wa Jiji la Dar es salaam na kuzungumza nao kupitia mada za kuwajengea uwezo na kutambua thamani ya uingizaji na umuhimu wa weledi katika uingizaji.

“Kupitia kongamano hili wasanii watajifunza mambo mengi ikiwemo uandishi wa miswada na umuhimu wa utafiti, kutengeza Brand, kujitangaza, usimamizi pamoja na uongozaji wa filamu,” alisema Fissoo.

Akizitaja mada zitakazotolewa katika kongamano hilo ni pamoja matumizi ya mitandao ya kijamii, elimu ya mapambano dhidi ya rushwa, athari za madawa ya kulevya kwa wanatasnia wa filamu pamoja na uandishi wa mikataba .

“Kongamano hili ni muhimu sana kwa waingizaji wote wa Jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu hivyo tunaomba wasanii wote wajitokeze kwa wingi zaidi kwani filamu ni ajira, filamu ni uchumi kwa maendeleo ya viwanda,” alisema Fissoo.

Hata hivyo alisema katika kongamano hilo viongozi wa dini watakuwepo na kutoa elimu kuhusiana na maadili katika filamu na tamthilia za kitanzania.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa TDFAA, Jimmy Mafufu alisema wasanii wengi wamekuwa wakipata fedha nyingi katika kazi zao lakini wanashidwa namna ya kuzitumia kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha.

“Wasanii wengi wamekuwa wakitumia fedha zao kwa ajili ya kununulia magari ya kufahari huku wakiishia katika nyumba za kupanga na kuishi maisha ya kuzalilika…hivyo kupitia kongamano hili tutaweza kuelimika zaidi” alisema Mafufu.

(Visited 241 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us