ASSAs

RAIS MAGUFULI AWAPA SOMO ZITO WANAFUNZI MKOANI NJOMBE

1083
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa wanafunzi kutulia na kutilia mkazo katika masomo na kuacha mambo yasiyofaa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza  kwenye ziara yake inayoendelea mkoani  Njombe.

na nyinyi watoto muache viherehere nawaambia ukweli wanangu, mtu anakwambia ninakupandisha pikipiki, acheni viheherere wewe kama bado ni mdogo tulia kwanza utavikuta, utavikimbia mwenyewe na utavichoka, pata elimu yako kwanza utakuja kumchagua unayemtaka.” amesema Rais Magufuli.

Amewaagiza kama atakuwepo yeyote atakaye wasumbua wakiwa bado masomoni basi wasisite kumlipoti katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mtu akikutongoza anakufuatilia sana mpeleke kwa Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Wilaya sema huyu kila siku ananitongoza.”, ameongeza Rais Magufuli.

Rais Magufuli kwa sasa anafanya ziara mkoani Njombe ambapo atazindua miradi mbalimbali, ikiwemo ya barabara pamoja na ujenzi wa hospitali.

(Visited 77 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us