ASSAs

BALOZI WA UFARANSA AWAFUTA JASHO WAANDISHI WA HABARI

1034
0
Share:

Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier ameguswa na kasi ya uwajibikaji wa Vyombo vya Habari nchini unaojikita katika misingi ya kuchochea maendeleo, ambapo amewatia moyo wanahabari kutokana na chamngamoto wanazopitia.

Clavier amesema changamoto iliyopo ni pamoja na mapinduzi ya kiteknolojia yaliyoingia katika kipindi hiki na kuathiri mfumo wa habari zinazoenda kwa jamii bila kujali nzuri au mbaya.

Amezungumza hayo alipokuwa katika hafla ya wanahabari iliyofanyika nyumbani kwa balozi huyo jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya shukrani kutokana na kazi wanazozifanya wanahabari nchini.

“Mabadiliko haya yamekuja na changamoto mpya na majukumu mapya katika nchi zote duniani naamini vyombo vya habari vitafanya kazi kuitengeneza jamii iweze kuimarika katika misingi ya kimaadili.

Moja kati ya michango inayotolewa na Ufaransa kwa ajili ya kutimiza lengo hili ni uwapo wa kituo cha Radio Ufaransa na kuimarisha mahusiano ya kikazi” amesema Clavier.

Aidha amesema tangu alipoingia hapa nchini amebaini kuwapo na maendeleo mazuri katika mijadala kati ya Serikali na wadau wa vyombo vya habari kuhusiana na masuala ya haki za binadamu, Ulinzi katika Uhuru wa kujieleza na ukosoaji.

Ameongeza kuwa “wakati nikishuhudia majadiliano yakiendelea tunapenda kuwatoa hofu kwamba ubalozi wa Ufaransa unatoa ushirikiano katika majadiliano hayo ili kuhakikisha uchumi wa nchi amani na Ulinzi vinaendelea kuimarika”

(Visited 72 times, 1 visits today)
Share this post